Ziwa Peipus
Mandhari
| |
Nchi zinazopakana | Estonia, Urusi |
Eneo la maji | km2 3,555 |
Kina cha chini | m 15.3 |
Mito inayoingia | mito Emajõgi, Velikaya |
Mito inayotoka | mto Narva |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
m 30 |
Miji mikubwa ufukoni | Pskov |
Ziwa Peipus (kwa Kiestonia: Peipsi-Pihkva järv; kwa Kirusi: Чудско-Псковское озеро; kwa Kijerumani: Peipussee) ni ziwa kubwa la maji safi katika Ulaya ya Kaskazini. Liko kwenye mpaka baina ya Estonia na Urusi.
Ziwa Peipus ni ziwa la nne kubwa zaidi Ulaya likiwa na eneo la kilomita za mraba 3,500. Kina cha wastani ni mita 7, sehemu ndefu zaidi ni mita 15.
Ziwa hutumiwa kwa uvuvi na burudani.
Tarehe 5 Aprili 1442 ziwa hilo lilikuwa mahali pa mapigano ambayo ni mashuhuri katika historia ya Ulaya. Jeshi la Wamisalaba Wajerumani lilishindwa na jeshi la Warusi wa Novgorod na hivyo uenezi wa Dola la Wamisalaba Wajerumani ulisimamishwa. Mapigano yakitokea kwenye barafu ya Ziwa Peipus lililokuwa limeganda kutokana na baridi ya mwezi Aprili.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ziwa Peipus kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |