Wasimbiti
Mandhari
Wasimbiti ni kabila la Tanzania kaskazini, jamii ya Wakurya, pia wamechanganyika na Wajaluo.
Wanaishi kando ya Ziwa Viktoria katika wilaya ya Rorya karibu na mpaka wa Kenya na wa wilaya ya Musoma mjini. Mto Mara unakata vijiji kama vile Kirumi, Kuruya, Mbatamo, Kinesi, Nyamaguku au Iryenyi.
Wasimbiti wenyewe wanakadiriwa kuwa watu 33,000 hivi, pamoja na vikundi walio karibu na kuelewana nao kilugha kama vile Wahacha, Wakine, Wakiroba, Wasurwa na Wasweta wako zaidi ya laki 1.
Ndugu yao upande wa Kenya wanaitwa Wasuba.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Uchumi wao unategemea uvuvi, ufugaji na wengine ni wakulima pia. Mazao wanayolima ni mihogo, mahindi, viazi vitamu, mtama, mlezi n.k. Pia ni wawindaji.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kuhusu Wasimbiti Archived 7 Machi 2016 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wasimbiti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |