Nenda kwa yaliyomo

Mongolia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wamongolia)
Монгул Улс
Mongol Uls

Jamhuri ya Mongolia
Bendera ya Mongolia Nembo ya Mongolia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Dayar Mongol"
Wimbo wa taifa: Bügd Nairamdakh Mongol
Lokeshen ya Mongolia
Mji mkuu Ulaanbaatar
47°55′ N 106°53′ E
Mji mkubwa nchini Ulaanbaatar
Lugha rasmi KiMongolia
Serikali Demokrasia ya kibunge
Khaltmaagiin Battulga
Luvsannamsrain Oyun-Erdene
Uhuru
Kutangazwa
Kutoka Uchina
11 Julai 1921
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,564,116 km² (18th)
0.43
Idadi ya watu
 - Januari 2020 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
3,278,290 (134th)
2,650,952
1.97/km² (238th)
Fedha Tugrug (MNT)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC 7)
(UTC 8)
Intaneti TLD .mn
Kodi ya simu 976

-



Mongolia (kwa Kimongolia: Монгол Улс, mongol uls) ni nchi ya bara la Asia.

Imepakana na nchi za Urusi na Uchina.

Ni nchi kubwa ya 19 duniani lakini kuna wakazi wachache tuː jumla milioni 2.6 hivyo msongamano wa watu ni mdogo sana.

Sehemu za kusini mwa Mongolia ya kihistoria ziko ndani ya Jamhuri ya Watu wa China.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]
Ramani ya Mongolia

Mongolia ni nchi ya mbuga yabisi, majangwa na milima inayofikia kimo cha mita 4,374 juu ya UB (Nayramadlin Orgil).

Kaskazini mwa nchi kuna ardhi yenye hali ya sakitu ya kudumu yaani yenye halijoto chini ya 0 C° ndani yake isiyopoa hata wakati wa majira ya joto. Kusini kuna jangwa kubwa la Gobi.

Asilimia 10 pekee za nchi ina misitu hasa mlimani na ardhi inayolimika ni 1 % tu.

Hali ya hewa

[hariri | hariri chanzo]

Hali ya hewa ni ya kibara na ina tofauti kubwa. Majira hubadilishana kuwa na joto pia baridi kali. Wastani wa siku ni kati ya −25 °C na 20 °C. Hali halisi wakati wa joto mchana kuna joto kali lakini usiku huwa baridi.

Usimbishaji una tofauti kubwa kati ya kaskazini na kusini mwa nchi. Kusini ni yabisi zaidi hadi kushuka kwa mm 100 za mvua pekee kwa mwaka katika jangwa la Gobi.

Miji mikubwa ni mji mkuu Ulaanbaatar (Улаанбаатар) (takriban wakazi milioni moja - zaidi ya theluthi ya watu wote wa taifa), halafu Erdenet (wakazi 79,649), Darchan (72,386) na Choibalsan (44,367).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Miaka 800 iliyopita nchi hii ilikuwa chanzo cha moja kati ya milki kubwa kabisa katika historia wakati ambako Chingis Khan alipounda Milki ya Wamongolia iliyoenea kuanzia China hadi Mashariki ya Kati na Ulaya.

Hadi mwaka 1992 nchi iliitwa Jamhuri ya Watu wa Mongolia na kufuata sera za ukomunisti.

Wakazi ni hasa Wakhalkhas (82%), Wakazaki (4%) na wengineo.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kimongolia.

Upande wa dini, Wabuddha ni 53%, Waislamu ni 3%, wafuasi wa dini za jadi ni 2.9%, Wakristo ni 2.2%, lakini 38.6% hawana dini yoyote.

Uchumi wa Mongolia hutegemea hasa migodi na ufugaji. Kihistoria Wamongolia walikuwa wafugaji waliohamahama na wanyama wao na kuishi katika hema. Tangu mapinduzi ya mwaka 1921 sekta ya migodi na viwanda ilijengwa.

Sekta ya kisasa ya biashara iko hasa kwenye mji mkuu.

Hadi leo karibu nusu ya wakazi huishi nje ya miji wakifuatana na wanyama wao ambao ni hasa kondoo, mbuzi, ng'ombe, farasi na ngamia.

Kilimo kipo mahali pachache kufuatana na tabia yabisi ya nchi. Wakati wa baridi sehemu kubwa ya wafugaji hukaa vijijini walipojenga nyumba.

Migodi ni hasa makaa mawe, shaba, bai na dhahabu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
General information
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mongolia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.