Volta (mto)
Mandhari
(Elekezwa kutoka Volta)
Chanzo | maungano ya mito ya Muhun, Nazinon na Nakambe karibu na mji wa Salaga (Ghana) |
Mdomo | Bahari ya Atlantiki |
Nchi | Ghana |
Urefu | 2,574 km pamoja na tawimto wa Muhun (Volta Nyeusi) |
Kimo cha chanzo | 180 m kwenye maungano ya mito |
Volta ni mto muhimu wa Afrika ya Magharibi. Inaanza katika maungano ya matawimto yake ya Muhun (Volta nyeusi), Nazinon (Volta nyekundu) na Nakambe (Volta nyeupe) karibu na mji wa Salaga, Ghana.
Katika Ghana boma la lambo la Akosombo (Ghana) limesababisha kutokea kwa ziwa Volta ambalo ni lambo kubwa kabisa duniani. Baada ya kuondoka katika ziwa hilo lisilo asilia Volta inaingia katika Ghuba ya Guinea ya bahari Atlantiki.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Volta (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |