Victor Wembanyama
Victor Wembanyama (amezaliwa 4 Januari 2004) ni mchezaji wa Ufaransa anayecheza mpira wa kikapu huko Metropolitans 92 ya LNB Pro A. Anakadiriwa sana kuchaguliwa na timu ya San Antonio Spurs kama chaguo nambari moja katika drafti ya Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) ya 2023 na anakadiriwa kuwa mmoja wa matarajio makubwa ya mpira wa kikapu wakati wote.[1][2][3]
Ni mzaliwa wa Le Chesnay, Ufaransa, Wembanyama alianza taaluma yake na timu ya Nanterre 92 ya LNB Pro A mnamo 2019. Miaka miwili baadaye, alihamia ASVEL na kushinda taji la Pro A katika msimu wake wa kwanza akiwa na timu hiyo. Mnamo 2022, Wembanyama alitia saini na Metropolitans 92 na kuchukua jukumu la uongozi. Amechaguliwa kuwa nyota wa LNB (All-Star) mara mbili, akishinda tuzo ya mchezaji mwenye dhamani zaidi katika mchezo wa nyota(mastaa) wa ligi ya LNB (All-Star Game MVP) mara moja, na ni Mchezaji Bora Chipukizi wa LNB Pro A mara mbili.
Wembanyama anachezea timu ya taifa ya Ufaransa ya mpira wa kikapu. Katika ngazi ya vijana, ameiongoza timu yake kutwaa medali mbili za fedha, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia la FIBA chini ya umri wa miaka-19 2021, ambapo aliweka rekodi ya FIBA ya kuzuia kufungwa katika kila mchezo (blocks per game) kwenye shindano moja tu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "2023 NBA Draft Lottery: Meet Victor Wembanyama, the best prospect since LeBron James, projected to go No. 1". Yahoo Sports (kwa American English). 2023-05-16. Iliwekwa mnamo 2023-05-25.
- ↑ Adam Zagoria. "18-Year-Old Frenchman Victor Wembanyama Being Hailed As The 'Single Greatest Prospect In NBA History'". Forbes (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-05-25.
- ↑ Draft Digest Staff (2023-05-12). "2023 NBA Draft: Is Victor Wembanyama the Best Prospect We've Ever Seen?". NBA Draft Digest - Latest Draft News and Prospect Rankings (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-05-25.