Utenzi wa Mwanakupona
Utenzi wa Mwanakupona ni kati ya tenzi za Kiswahili zilizohifadhiwa tangu karne ya 19. Ilitungwa mnamo mwaka 1858/1860 na Mwanakupona binti Mshamu Nabhany, mke wa sultani wa Siu, akimuandikia mtoto wake wa kike aliyekuwa akiitwa Mwana Hashima bint Shee aliyeishi kati ya mwaka 1841 hadi 1931 [1] [2]. Utenzi huo uliandikwa kwa mwandiko wa Kiarabu, jinsi iliyokuwa kawaida kwa Kiswahili wakati ule.[3]
Kuanzia miaka ya 1890 utenzi huu ulianza kuchapishwa huko Ulaya katika hati za Kirumi, lakini matoleo ambayo yaliweza kuhifadhika ni kuanzia yale ya mwaka 1930 hadi leo.
Mwaka 1962 Lyndon Harries alichapisha toleo jingine la utenzi huu.
Utenzi huu ni wa mawaidha kwa msichana ukimfunza namna ya kuishi katika maisha ya kinyumba na ya kijamii na una jumla ya beti zipatazo mia moja na mbili, ukiwa ni utenzi unaofanana kidogo kimawaidha na utenzi wa Howani Mwana Howani ulioandikwa mwaka 1983 na Zaynab Himid Mohamed ambazo tenzi zote mbili zinazungumzia sana maisha ya mtoto wa kike, kijamii na kidini [4]
Katika utenzi huu, mtunzi anaanza kumuita binti yake akaribie akiwa na wino na karatasi ili asikilize wosia, anamueleza binti yake kuwa yeye ni mgonjwa na alikuwa hajapata nafasi ya kumpa mawaidha. Anamwambia binti yake apende kumtukuza Mungu na kumuomba rehema zake, baada ya hapo anamwambia anataka kumpa hirizi ili iwe kinga yake na hirizi yenyewe ndiyo utenzi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tenzi tatu za kale. Mulokozi, M. M. (Mugyabuso M.), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Dar es Salaaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. 1999. ISBN 9976-911-34-3. OCLC 45248518.
{{cite book}}
: CS1 maint: others (link) - ↑ http://journals.udsm.ac.tz/index.php/mj/article/view/1620/1515
- ↑ Angalia muswada mojawapo hapa Utenzi wa Mwana Kupona Ilihifadhiwa 31 Januari 2020 kwenye Wayback Machine., tovuti ya Digital Collections ya SOAS, Chuo kikuu cha London
- ↑ Mohammed, Zaynab Himid. (2004). Howani mwana Howani : tenzi za Zaynab Himid Mohammed. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. ISBN 9776911645. OCLC 144607717.
{{cite book}}
: Check|isbn=
value: checksum (help)
Maandiko kuhusu Utenzi wa Mwanakupona
[hariri | hariri chanzo]- Muhamed Seif Khatib: Utenzi wa Mwanakupona, makala katika Mulika Na. q7-1985, Jarida la Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili, Dar es Salaam.
- Uchambuzi wa Utenzi wa Mwanakupona: mawaidha katika tendi, blogu ya Mwalimu wa Kiswahili, November 21, 2017 online hapa Ilihifadhiwa 31 Januari 2020 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Utenzi wa Mwanakupona kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |