Nenda kwa yaliyomo

Utashi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utashi, sanamu ya Louis-Charles Janson kwa Opéra national de Paris (1875).

Utashi (kwa Kiingereza: will) ni kipawa cha binadamu kinachomfanya aweze kutaka mwenyewe chochote.

Kitu hicho kinaweza kuwa chema na hata kibaya, ingawa akili yake mwenyewe inaona zaidi wema fulani uliomo na ambao unamvuta.

Katika dunia hii binadamu ndiye kiumbe pekee mwenye utashi, nao huongeza sifa ya utambuzi wa mvuto wa kilicho chema katika ubaya au kilicho kibaya katika wema, kuchagua na kupanga kwa kuzingatia yaliyopita na matamanio katika wakati ujao, kuunda mambo mapya, na kutamani kurekebisha mambo kwenda katika hali bora zaidi.