Nenda kwa yaliyomo

Under Pressure

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

"Under Pressure" uliotungwa na kutayarishwa na bendi ya Queen na David Bowie. Wimbo huu uliandikwa kwa pamoja na Freddie Mercury, Brian May, Roger Taylor na John Deacon wote wakiwa wanachama wa bendi ya Queen. Kwa ushirikiano wa pamoja na David Bowie. Ulirekodiwa katika studio ya Mountain Studios huko Montreux, Uswisi—mnamo mwaka 1981.

Wimbo huu ulitolewa kama single mnamo Novemba 1981. Ulikuwa na mafanikio makubwa kwenye chati za muziki. Ulifikia nafasi ya kwanza kwenye chati za muziki nchini Uingereza na nafasi ya 29 kwenye chati za Billboard Hot 100 huko nchini Marekani.

Katika miaka iliyofuata, kipande maarufu cha bassline cha wimbo huu kilikopiwa na msanii Vanilla Ice kwenye wimbo wake "Ice Ice Baby" wa mwaka 1990. Hata hivyo, hakuomba ithibati ya kutumia kipande hicho. Kitu ambacho kilililosababisha mashtaka ya kisheria kutoka kwa Queen na David Bowie. Hatimaye, suala hilo liliamuliwa nje ya mahakama ambapo Vanilla Ice alilazimika kulipa fidia na kutoa ithibati rasmi kwa Queen na David Bowie kama wamiliki wa asili wa kipande hicho.

"Under Pressure" umeendelea kuwa na athari kubwa katika ulimwengu wa muziki na utamaduni wa pop. Ukitumiwa mara nyingi katika filamu, matangazo, na matukio mbalimbali ya kitamaduni. Ni moja ya nyimbo zinazothaminiwa sana katika historia ya muziki, ikiendelea kuvutia mashabiki wapya na wa zamani.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]



Makala hii ni sehemu ya mradi wa kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari.