Sun City, Kaskazini Magharibi
Sun City ni hoteli na kasino ya kifahari nchini Afrika Kusini, iliyoko katika Mkoa wa Kaskazini Magharibi wa Afrika Kusini. Mwendo wake ni karibu masaa mawili kwa gari kutoka Johannesburg, karibu na mji wa Rustenburg. Inapakana na Mbuga ya Kitaifa ya Pilanesberg
Historia
[hariri | hariri chanzo]Sun City ilianzishwa na gwiji wa biashara za hoteli Sol Kerzner kama sehemu ya kundi lake la mali la Sun International. Ilifunguliwa rasmi tarehe 7 Desemba 1979; wakati huo ilikuwa iko katika eneo la bantustan la Bophuthatswana.
Kwa sababu Jimbo la Bophuthatswana lilikuwa limetangazwa kuwa huru na serikali ya ubaguzi wa rangi ya Afrika Kusini (ingawa halikuwa limetambulika na mataifa mengine), liliruhusiwa chini ya sheria ya Afrika Kusini wakati huo kutoa burudani kama kamari na maonyesho ya uchi, ambayo ilikuwa marufuku katika Afrika Kusini. Sababu hizi, vilevile na ukaribu wake kwa maeneo makubwa ya miji mikuu ya Pretoria na Johannesburg, zilihakikisha kuwa Sun City ilikuwa (na ilisalia) hoteli mashuhuri kwa likizo na wikendi. Wanamuziki wengi maarufu kama Queen, Elton John,Linda Ronstadt , Julio Iglesias, The O'Jays, Ray Charles, Boney M.,Black Sabbath, Rod Stewart, Tina Turner, Dionne Warwick, Sarah Brightman, Laura Branigan na Thomas Anders (wa Modern Talking fame) pia walitumbuiza katika 'Sun City Super Bowl', ambayo ina viti 6230. Sun City pia ilikuwa mahala pa kuchezewa mechi za Ndondi za Uzani Mzito katika miaka za 1970 na mwanzo wa miaka ya 1980. Bondia mmoja ni Gerrie Coetzee, ambaye baadaye (1981) ilikuwa bingwa wa dunia wa Heavyweight .
Akizungumza katika miaka ya 1980 na Jani Allan wa Sunday Times , Kerzner alielezea mkakati wake; "Unatazama hatari ...Piga hesabu ya hatari, fanya utafiti wa soko ya Kimataifa vyema, tambua ladha, mtindo, hamu na starehe za watu wa Afrika Kusini, lenga kuwapa starehe mzuri kwa bei wanaimudu - halafu tekeleza."
Sun City ikawa mahali penye utata mwaka wa 1985 wakati mpiga gitaa wa bendi ya E Street Band Steven Van Zandt aliifanya pa muziki wa kundi lake la wanaharakati , Artists United Against Apartheid. Wasanii arobaini na tisa mashuhuri walishirikiana kurekodi wimbo wa "Sun City", ambao waliapa kutotumbuiza katika hoteli hiyo. Kuongezea, Simple Minds, katika albamu yao "Live in the City of Light" iliyotolewa mwaka wa 1987,walijumuisha wimbo ulioitwa "Love Song - Sun City - Dance to the Music" walikotangaza wao " hawawezi kutumbuiza katika Sun City".
Kipindi cha Baada ya Ubaguzi wa rangi
[hariri | hariri chanzo]Sun City imeendelea kustawi tangu mara Bophutatswana ilingizwa tena upya katika Afrika Kusini mwaka wa 1994.
Kundi hili lina hoteli nne:
- Hoteli ya Sun City;
- Hoteli ya Cascades;
- The Cabanas;
- The Palace of the Lost City.
Kwa kuongeza katika hoteli ya nne, sehemu hii inajumuisha vifaa vya kushiriki inayoitwa "The Sun City Vacation Club" ambayo ni maarufu kwa upishi wa kujitegemea upishi.
Sun City pia ina kozi 18 za kimataifa za mchezo wa golf ,Gary Player Country Club na Lost City Golf Course, zote ambazo zilipangiliwa na Gary Player. Gary Player Country Club ni nyumbani kwa pambano la kifahari la Nedbank Golf Challenge (zamani ikiwa Nedbank Dollar Milioni Golf Challenge), wakati Lost City Golf Course inajulikana kwa mamba 38 wa ukweli katika kipengele cha maji cha shimo la 13 .
Hoteli hii pia ilikuwa mahali pa Mkataba wa Sun City.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Sun International Website Ilihifadhiwa 17 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.