Nenda kwa yaliyomo

Shiva

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Hekalu katika hekalu ya Bangalore

Shiva ni mmoja kati ya miungu wakuu katika dini ya Uhindu.

Katika mafundisho ya Trimurti inayolenga kuunganisha pande zote za Uhindu Shiva ni mmoja kati ya miungu mikuu 3. Hapa nahusika kazi ya kubadilisha dunia na kuiharibu kwenye mwisho wa wakati wake.

Katika dhehebu kubwa ya Ushiva anaabudiwa kama mungu mkuu, muumba na mlinzi dhidi ya maovu yote.

Anaonyesha mara nyingi katika hali ya kutafakari na kusali kama yogi. Mungu mwenzake wa kike ni Parvati. Ganesha na Kartikeya ni wana wake. Hupanda n'gombe dume anayejulikana kwa jina Nandi.

Shiva huonyeshwa mara nyingi kwa shingo ya buluu kwa sababu kutokana na masimulizi ya Kihindi aliokoa dunia safari moja kwa kunywa sumu. Huwa na macho matatu na jicho la tatu liko katikakati ya kidundu chake.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.