Rivaldo
Rivaldo (alizaliwa 19 Aprili 1972) alikuwa mchezaji wa soka wa timu ya taifa ya Brazili na klabu ya Barcelona F.C. ya nchini Hispania aliyekuwa anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji.
Kabla ya kwenda Barcelona aliichezea timu ya klabu ya Deportivo La Coruña ya nchini Hispania kuanzia mwaka 1996 hadi 1997.
Mwaka 1997 alihamia klabu ya Barcelona na kucheza kwa mafanikio makubwa ambapo mwaka 1999 walifanikiwa kuchukua makombe mawili ya LA LIGA na Copa del Rey na kufanikiwa kufunga magoli 19 katika mechi 34 na kufanikiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa FIFA na Ballon d'Or.
Mwaka 2002 Rivaldo alihamia timu ya klabu ya AC Milan ya nchini Italia na kufanikiwa kubeba mataji mawili ya Coppa italy na UEFA.
Kwa sasa Rivaldo ni rais wa timu ya klabu ya Mogi Mirim Esporte Clube ya nchini Brazili.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rivaldo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |