Richard Limo
Rekodi za medali | ||
---|---|---|
Richard Limo (Kushoto) katika Amsterdam Marathon mwaka wa 2007 | ||
Men’s Wanariadha | ||
Anawakilisha nchi Kenya | ||
World Championships | ||
Dhahabu | 2001 Edmonton | 5,000 m |
Richard Kipkemei Limo (alizaliwa mnamo 18 Novemba 1980) mwanariadha kutoka taifa la Kenya. Yeye ni mtaalamu katika matukio ya masafa marefu. Alishinda medali ya dhahabu katika mita 5000 katika mchuano wa dunia katika riadha mwaka wa 2001.
Alizaliwa mwaka wa 1980 katika kijiji cha Cheptigit, wilayani Uasin Gishu. Baada ya shule ya msingi alihudhuria Polytechnic na kupokea daraja katika masomo ya waya na umeme mwaka wa 1996. Hakuwa ameanza kukimbia hadi mwaka wa 1997 wakati alijiunga na kambi ya mafunzo iliyoko karibu na nyumbani kwake. Mwaka uliyofuata alishinda medali ya fedha katika mbio ya vijana katika mchuano wa World Cross Country. Mwaka huo huo alivunja rekodi ya dunia ya vijana katika[mita 3000 kwa kukimbia kwa muda wa dakika 7:36.76, lakini alikosa mchuano wa dunia wa vijana. Mwaka wa 2001 akawa bingwa wa dunia na pia akawa mtendaji bora duniani wa mwaka huo ambao ulikuwa mwaka wa 2001 katika mbio za mita 5000 na muda wake wa dakika 12:56.72, bado ni rekodi yake bora ya kibinafsi. Tangu mwaka wa 2004 hajakuwa akionekana sana na vyombo vya habari, lakini tangu wakati huo amebadilika na kuanza kukimbia mbio ya masafa marefu zaidi ya marathon. Alichukua nafasi ya pili mwaka wa 2007 katika Amsterdam Marathon, mbio yake ya marathon ya kwanza ambapo rekodi yake bora na mpya ya kibinafsi (masaa 2:06:45)
Alimwoa kipenzi chake cha moyo Rose Tarus na wana watoto wawili, ambao walizaliwa miaka 2000 na 2002. Ana urefu wa mita 1.67 na uzito wa kilogramu 52. Hana uhusiamo wowote na Benjamin Limo au Felix Limo, ambao ni wanariadha wa nchi ya Kenya.
Majalio
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Mchuano | Ukumbi | Nafasi | Ziada |
---|---|---|---|---|
1998 | Mashindano ya dunia ya Cross Country | Marrakech, Moroko | 2 | Junior |
Michezo ya Jumuiya ya Madola | Kuala Lumpur, Malaysia | 3 | mita 5000 | |
Mashindano ya Kiafrika | Dakar, Senegal | 2 | mita 3000 | |
1999 | Mashindano ya dunia ya Cross Country | Belfast, Ireland ya Kaskazini | 2 | Ya vijana |
Michezo ya All-Africa | Johannesburg, Afrika Kusini | 6 | mita 5000 | |
2000 | Michezo ya Olimpiki | Sydney, Australia | 10 | mita 5000 |
2001 | Mashindano ya dunia ya Cross Country | Oostende, Ubelgiji | 32 | Ya umbali |
Mchuano wa dunia | Edmonton, Kanada | 1 | mita 5000 | |
Fainali ya IAAF Grand Prix | Melbourne, Australia | 5 | mita 5000 | |
2002 | Mashindano ya dunia ya Cross Country | Dublin, Ireland | 4 | Ya urefu |
IAAF Grand Prix Final | Paris, Ufaransa | 7 | mita 5000 | |
mwaka wa(2003). | Mashindano ya dunia ya Cross Country | Lausanne, Uswisi | 4 | Ya urefu |
IAAF World Athletics Final | Monako | 2 | mita 5000 | |
2004 | Mashindano ya dunia ya Cross Country | Brussels, Ubelgiji | 32 | Ya urefu |
Mbio za marathon
[hariri | hariri chanzo]- 2007 Amsterdam Marathon - 2 (AS 2:06:45)
- 2008 Rotterdam Marathon - 4
- 2008 Chicago Marathon] - 10
- 2009 Rotterdam Marathon - 9 [1]
Ubora wa kibinafsi
[hariri | hariri chanzo]- Mita 1500 - dakika 3:37.59 (1999)
- Mita 3000 - dakika 7:32.23 (2001)
- Mita 5000 - dakika 12:56.72(2001)
- 10,000 mita - dakika 26:50.20 (2002)
- Steeplechase mita 3000 - dakika 8:20.67 (1998)
- Marathon - 2:06.43 (2007, muda: 2:06.45)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ IAAF, 5 Aprili 2009: Kibet edges Kwambai kama wote clock 2:04:27 - Rotterdam ripoti Marathon
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- IAAF wasifu wa Richard Limo
- Richard Limo: Young Kenyan on Top of the World Archived 6 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
- Focus on Africans
- Marathoninfo profile
Sporting positions | ||
---|---|---|
Alitanguliwa na Brahim Lahlafi |
Men's 5,000 m Best Year Performance 2001 |
Akafuatiwa na Salah Hissou |