Nenda kwa yaliyomo

Rembrandt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rembrandt van Rijn)
Alivyojichora mwaka 1661

Rembrandt Harmenszoon van Rijn (15 Julai 16064 Oktoba 1669) alikuwa mchoraji mashuhuri nchini Uholanzi wakati wa karne ya 17.

Alizaliwa mjini Leyden kama mtoto wa tisa wa msagi Harmen Gerritszoon van Rijn na mke wake Cornelia Neeltgen Willemsdochter van Zuytbrouck.

Alianza kuchora akiwa bado mtoto na mwanafunzi. Baada ya kumaliza shule alianza masomo kwenye chuo kikuu cha Leyden lakini aliacha masomo, badala yake aliingia katika mafunzo kwa mchoraji Jacob van Swanenburgh mjini Leyden.

"Walinzi wa Usiku" walivyochorwa na Rembrandt

Tangu mwaka 1631 alihamia Amsterdam alipopata wateja wengi waliomwajiri kuchora picha zao. Huko mwaka 1634 alimwoa Saskia van Uylenberg akazaa naye watoto wanne, lakini ni mmoja tu aliyeishi na kufikia umri mkubwa.

Katika sanaa yake alipata umaarufu kutokana na umakini wa picha zake. Alijua kucheza na giza na mwanga na picha ya "Walinzi wa Usiku" ni mfano bora.

Picha zake mwenyewe

[hariri | hariri chanzo]

Picha nyingine

[hariri | hariri chanzo]