Rebeca Andrade
Rebeca Rodrigues de Andrade (amezaliwa 8 Mei 1999) [1] ni mtaalamu wa mazoezi ya viungo, mwenye uraia wa Brazili na Mwana Olimpiki mara mbili, akiwa amewakilisha Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki ya 2016 na 2020. Yeye ni bingwa wa Olimpiki wa 2020, bingwa wa ulimwengu wa 2021, mshindi wa medali ya fedha ya Olimpiki ya 2020, na bingwa wa pande zote wa 2021 wa Pan American. Alikuwa mwanachama wa timu zilizoshinda dhahabu katika Mashindano ya Pan American 2018 na fedha ya 2021. [2] Andrade ndiye mwana mazoezi ya viungo wa kike wa kwanza wa Brazili kupata medali katika Michezo ya Olimpiki na mshindi wa kwanza wa medali ya Olimpiki ya pande zote aliyefuzu pekee.
[3] Pia yeye ni mwanamke wa pili kutoka Brazili kushinda medali ya dhahabu katika Mashindano ya Ulimwengu ya Mazoezi ya Kisanaa. [4]
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Rebeca Andrade alizaliwa tarehe 8 Mei 1999 huko Guarulhos. Yeye ni mmoja wa watoto wanane wa mama asiye na mume, pia mama yake aliuza vitu vya ndani vya nyumba na kutembea hadi kazini ili kulipia mafunzo ya Rebeca ili atimize ndoto zake. [5] Alianza mazoezi ya viungo alipokuwa na umri wa miaka minne baada ya shangazi yake kumpeleka kwenye jumba la mazoezi ambapo alipokua anafanyia kazi.[6] Mama yake Rebeca anazungumza lugha ya Kireno na Kiingereza.[7] Yeye ni Mwafro-Brazil. [8] [9]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.olympedia.org/athletes/129288
- ↑ https://www.uol.com.br/esporte/colunas/olhar-olimpico/2021/06/05/rebeca-andrade-conquista-vaga-olimpica-e-vai-levar-baile-de-favela-a-toquio.htm
- ↑ https://www.nytimes.com/2021/07/29/sports/olympics/rebeca-andrade-is-the-first-brazilian-to-win-any-medal-in-womens-gymnastics.html
- ↑ https://apnews.com/article/sports-china-japan-asia-tokyo-315e93983f8b9b34e0a8eb180df5e202
- ↑ https://www.npr.org/2021/08/01/1023393407/gymnast-rebeca-andrade-won-gold-for-brazil-and-became-a-national-hero
- ↑ https://www.gymnastics.sport/site/athletes/bio_detail.php?id=37359
- ↑ https://www.gymnastics.sport/site/athletes/bio_detail.php?id=37359
- ↑ https://www.npr.org/2021/08/01/1023393407/gymnast-rebeca-andrade-won-gold-for-brazil-and-became-a-national-hero
- ↑ https://www.npr.org/2021/08/01/1023393407/gymnast-rebeca-andrade-won-gold-for-brazil-and-became-a-national-hero