Nenda kwa yaliyomo

Pigmenti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nuru ambayo ni mchanganyiko wa mawimbi wa urefu mbalimbali unafika kwenye uso wa gimba; pigmenti inasharabu (kumeza) sehemu ya mawimbi haya na kuakisisha aina moja ya mawimbi tu hivyo kufanya gimba kuonekana kwa rangi fulani

Pigmenti ni dutu inayobadilisha rangi ya nuru kwa kusharabu sehemu za spektra.

Pigmenti hutumiwa kubadilisha kuonekana kwa rangi za kupakia, plastiki, madawa au wino.

Kuna pigmenti za kibiolojia kwa mfano kiwiti katika majani kinacholeta rangi ya kibichi, au melanini inayoamulia rangi ya ngozi, nywele na macho.