Kizole
Mandhari
(Elekezwa kutoka Onychognathus)
Kizole | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi = 11:
|
Vizole ni ndege wadogo kiasi wa jenasi Onychognathus katika familia Sturnidae. Wanatokea Afrika tu isipokuwa kizole Somali na kizole Arabu ambao wanatokea nchi za kiarabu pia. Wanapenda kuwa kwa makundi. Ndege hawa wana mabawa mekundu yaonekanayo sana wakiruka anwani. Manyoya ya dume ni meusi na yale ya jike yana rangi ya kijivu cheusi. Hula wadudu na matunda hasa, lakini hula nusra kila kitu. Hulijenga tago lao juu ya kipande cha jabali kilichojitokeza nje katika mahali penye kulindwa. Kizole mabawa-mekundu hutaga mijini pia juu ya vishubaka au mahali pengine penye kulindwa. Jike huyataga mayai 2-4 buluu.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Onychognathus albirostris, Kizole Domo-jeupe (White-billed Starling)
- Onychognathus blythii, Kizole Somali (Somali Starling)
- Onychognathus frater, Kizole wa Sokotra (Socotra Starling)
- Onychognathus fulgidus, Kizole Mabawa-kahawia (Chestnut-winged Starling)
- Onychognathus morio, Kizole Mabawa-mekundu (Red-winged Starling)
- Onychognathus nabouroup, Kizole wa Naburupi (Pale-winged Starling)
- Onychognathus neumanni, Kizole wa Neumann (Neumann's Starling)
- Onychognathus salvadorii, Kizole Utosi-mahameli (Bristle-crowned Starling)
- Onychognathus tenuirostris, Kizole Domo-jembamba (Slender-billed Starling)
- Onychognathus tristramii, Kizole Arabu (Tristram's Starling)
- Onychognathus walleri, Kizole wa Waller (Waller's Starling)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kizole wa Sokotra
-
Kizole wa Naburupi
-
Kizole utosi-mahameli
-
Kizole domo-jembamba
-
Kizole-jabali