Nzi-vunjajungu
Nzi-vunjajungu | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Pseudoclimaciella sp.
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Nusufamilia 4:
|
Nzi-vunjajungu ni wadudu wadogo kiasi wa familia Mantispidae katika oda Neuroptera (wadudu mabawa-vena) ambao wana miguu ya mbele inayofanana na ile ya vivunjajungu.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Nzi-vunjajungu wana urefu wa kati ya mm 5 na 47 na wana upana wa mabawa wa mm 5-30. Kadhaa, kama spishi za Pseudoclimaciella, huiga nyigu, lakini wengi sana ni hudhurungi pamoja na rangi za kijani, njano na pengine nyekundu. Majina ya kienyeji na ya kisayansi yametokana na muonekano wao wa vivunjajungu, kwani miguu yao ya mbele yenye miiba imetoholewa ili kukamata mawindo ya wadudu wadogo na inafanana sana na miguu ya mbele ya vivunjajungu (tofauti pekee ni kwamba vibano hukosa nyayo na havitumiwi kutembea kabisa). Wana mabawa manne kama viwambo ambayo yanaweza kuwa na ruwaza pengine (haswa katika spishi zinazoiga nyigu) lakini kwa kawaida huwa mangavu.
Wapevu ni wadudu mbuai ambao hukiakia usiku mara nyingi na huvutiwa pengine na taa. Hujilisha kwa wadudu wenye ukubwa unaofaa, ambao huwakamata kama vile vivunjajungu. Walakini, mifumo ya msingi ya mwenendo wa kukamata mawindo ni tofauti kati ya nzi-vunjajungu na vivunjajungu. Nzi-vunjajungu ni wawindaji wamilifu, lakini kama ilivyo na Neuroptera wengine, huruka kwa ugumu.
Lava wa Symphrasinae ni vidusia vya kukaa juu ya lava wa nyuki, nyigu au bungo-mavi. Lava wa Calomantispinae ni mbuai wa arithropodi wadogo, mara nyingi lava wao. Mantispinae wana maendeleo maalumu zaidi ya lava kati ya nzi-vunjajungu wote wanaochunguliwa hadi leo (historia ya maisha ya Drepanicinae bado haijulikani): lava wao hutafuta buibui wa kike au vifuko vyao vya mayai ambayo huingia kujilisha kwa mayai. Lava wa hatua ya kwanza wa mantispinae wanafanana na wadudu mikia-miwili (campodeiform: umbo la Campodea). Wanatumia mikakati miwili kupata mayai ya buibui: wanaweza kupenya moja kwa moja hariri ya vifuko vya mayai wanavyopata, au wanaweza kupanda na kubebwa na buibui wa kike kabla ya uzalishaji wa kifuko (phoresy) na huingia kwenye kifuko wakati kinapojengwa. Lava wanaopanda buibui huchukua nafasi kwenye au karibu na pediseli kwa kawaida; spishi fulani zinaweza kuingia kwenye mapafu-kitabu ya buibui. Wanajitunza juu ya buibui kwa kujilisha kwa hemolimfi yake. Uhamisho wa lava kutoka buibui hadi buibui unawezekana wakati wa kupandana au wa ulaji wa wenzao. Vikundi vikuu vyote vya buibui wawindao vinashambuliwa na nzi-vunjajungu wanaopanda buibui. Vifuko vya mayai vya spishi zinazojenga tandabui pia huingizwa na wapenyaji wa vifuko vya mayai. Ndani ya kifuko cha mayai lava hubambua kuwa na umbo linalofanana na mabuu ya bungo-mavi (scarabaeiform). Kisha huanza kujilisha kwa mayai wakitoa yaliyomo ndani yao kupitia mrija wa kutoboa/kufyonza ulioundwa kwa mandibula na maksila zilizotoholewa. Hatua ya mwisho inageuka kuwa bundo.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]
|
|
Jenasi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]
|
|
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Calomantispinae (Red-spotted mantidfly, Nolima pinal)
-
Drepanicinae (Ditaxis biseriata)
-
Mantispinae (Mantispa asphavexelte)
-
Symphrasinae (Theristria imperfecta)