Nenda kwa yaliyomo

Ngumi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngumi tayari
Ngumi ya salamu ya upinzani

Ngumi ni hali ya mkono ukifumbatwa, yaani kwa kukunja vidole pamoja na kiganja.

Kusudi la kukunja ngumi ni mara nyingi kupiga kwa nguvu, au kujiandaa kwa kupiga. Kutokana na maana hii ngumi inakunjwa pia kama alama ya hasira au ya upinzani, kwa mfano katika salamu ya Black Power.

Michezo ya mapigano mbalimbali hutegemea matumizi ya ngumi, hasahasa mchezo wa ngumi lakini pia karate au taekwondo.

Watafiti wamegundua ya kwamba kukunja ngumi inaweza kusaidia kuondoa hofu au wasiwasi kwa kuelekeza fikra kwa musuli na kuondoa fikra za wasiwasi.[1]

Kwa wtu wengine inaweza kusaidia pia kuelekeza fikra kwa jambo au kukumbuka habari.[2]


  1. "Clenched fist can help us deal with stress, scientists say". Telegraph. 2010-10-19. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-24. Iliwekwa mnamo 2013-05-05.
  2. Szalavitz, Maia (2013-04-29). "Clenching Fists Can Help Improve Memory, Researchers Find". Healthland.time.com. Iliwekwa mnamo 2013-05-05.


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: