Nenda kwa yaliyomo

Nembo ya Mexiko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya Taifa ya Mexiko
Tai anayeshika nyoka, kutoka maandishi ya Azteki kabla ya ukoloni


Nembo ya Mexiko inamwonyesha tai anayekalia mpungate na kushika nyoka. Mpungate unasimama kwenye mwamba.

Asili ya nembo ni katika utamaduni wa Azteki kabla ya kuingia kwa Wahispania nchini. Kuna hadithi ya kale juu ya kuundwa kwa Tenochtitlan ambayo ni mji wa Kiazteki uliotangulia Mexiko City.

Zamani ile Waazteki waliishi maisha ya kuhamahama na kutafuta mahali pa kujenga mji wa kudumu. Mungu wao Huitzilopochtli aliwaambia wamtafute anayekalia mpungate (kakati) na kushika nyoka. Mpungate utapatikana kwenye mwamba katika kisiwa ziwani. Hadithi yaendelea kusema ya kwamba baada ya matembezi ya miaka 200 walikuta ziwa la Texcoco penye mwamba na mpungate. Walipokaribia tai aliyeshika nyoka akaketi kenye mpungate huu.

Baada ya kupokea ishara hiyo waliunda mji wao wa Tenochtitlan uliokuwa baadaye mji mkuu wa Dola la Azteki na baada ya kuja kwa Wahispania mji wa Mexiko (Ciudad de México au Mexiko-City)

Nembo la kisasa lilichorwa 1968 na Francisco Eppens Helguera na kutangazwa kuwa nembo rasmi. Lakini nembo zote tangu uhuru zilionyesha tai na nyoka kwa namna moja au nyingine.