Usanifu majengo
Mandhari
(Elekezwa kutoka Msanifu)
Usanifu majengo ni sanaa na sayansi ya kubuni muundo na sura ya majengo. Sanaa na sayansi hii inajumuisha pia mambo kama mipango miji, usanifu wa eneo la kujenga, na hata ubunifu wa samani zitakazotumika ndani ya jengo.
Watu wanaojihusisha na haya huitwa "wasanifu majengo". Wanahitaji elimu ya ujenzi, hesabu, sanaa, teknolojia, elimu jamii na historia. Msanifu wa kwanza anayejulikana kwa jina ni Imhotep wa Misri ya Kale.
Mbinu za usanifu hutegemea teknolojia inayopatikana, hali ya hewa, hali ya jamii, utaratibu wa siasa yake, hali ya uchumi na mengine mengine.
Nchi na tamaduni mbalimbali ziliunda aina tofauti za usanifu majengo.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Usanifu majengo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |