Mkoa wa Pwani
Mkoa wa Pwani ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 61000.
Mkoa umepakana upande wa Kaskazini na Tanga, upande wa mashariki na Dar-es-Salaam na Bahari Hindi, upande wa kusini na mkoa wa Lindi na upande wa magharibi na mkoa wa Morogoro.
Makao makuu ya mkoa yako Kibaha.
Eneo na wakazi
Mkoa huu unalo eneo la km² 32,407, ukiwa na idadi ya wakazi wapatao 2,024,947 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1] kutoka 1,098,668 (2012).
Mkoa huu wenyeji wake ni watu wa makabila ya Wakwere, Wazaramo, Wandengereko, Wadoe, Wazigua na Wanyagatwa.
Wilaya ya Rufiji imegawanyika sehemu mbili, visiwani na bara: wenyeji wa visiwani ni wa kabila la Wanyagatwa na walio bara ndio Wandengereko. Wenyeji wa visiwani wanajishughulisha sana na uvuvi, kilimo cha mnazi na kupika chumvi, Wandengereko wanajishughulisha sana na mazao ya vyakula kama vile mpunga, mahindi n.k.
Wilaya
Mkoa wa Pwani una wilaya nane (katika mabano idadi ya wakazi wakati wa sensa ya mwaka 2022 [2]):
- Bagamoyo (205,478)
- Chalinze (316,759)
- Kibaha Mjini (265,360)
- Kibaha Vijijini (123,367)
- Kisarawe (159,226)
- Mkuranga (533,033)
- Mafia (66,180)
- Rufiji (159,906)
- Kibiti (195,638).
Mkoa huu una jumla ya majimbo ya uchaguzi yanayofikia (9) ambayo yanajumuisha Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kibaha Vijijini, Kibiti, Kisarawe, Mafia, Mkuranga na Rufiji [3]
Utalii
Mkoa huu ni maarufu sana kwa shughuli za kiutalii hususani katika mji wa Bagamoyo.
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Chalinze : mbunge ni Ridhwan Kikwete (CCM)
- Bagamoyo : mbunge ni Shukuru Kawambwa (CCM)
- Kibaha Mjini : mbunge ni Sylvester Francis Koka (CCM
- Kibaha Vijijini : mbunge ni Hamoud Abuu Jumaa (CCM)
- Kisarawe : mbunge ni Selemani Said Jafo (CCM)
- Mafia : mbunge ni Mbaraka Kitwana Dau (CCM)
- Mkuranga : mbunge ni Abdallah Hamis Ulega (CCM)
- Kibiti : mbunge ni Ally Seif Ungando (CCM)
- Rufiji : mbunge ni Mohamed Omary Mchengerwa (CCM)
Tazama pia
Tanbihi
- ↑ https://assengaonline.com/2022/11/05/matokeo-ya-sensa-2022-tanzania/
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Kuhusu majimbo linganisha Makadirio ya idadi ya watu katika majimbo ya uchaguzi Tanzania Bara kwa mwaka 2016: [http://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/majimbo/MAJIMBOApril_Kisw.pdf
Viungo vya nje
- Tovuti rasmi ya Mkoa wa Pwani, Tanzania
- (Kiingereza) Matokeo ya sensa 2002 kwa ajili ya mkoa wa Pwani
- Habari za Pwani kwenye kurasa za Tume ya Uchagizi Archived 21 Februari 2006 at the Wayback Machine.
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |