Nenda kwa yaliyomo

Mfumokleri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mfumokleri (au uklerikali au klerikalisimo) ni mazoea au utamaduni wa kuwaachia wakleri kuanzisha na kufanya karibu kila kitu katika Kanisa na hata katika siasa bila kushirikisha vya kutosha waumini wenzao, yaani watawa na hasa walei.

Jambo hilo linapingana na mtazamo sahihi unaoliona Kanisa kuwa familia ya Mungu ambamo wote ni ndugu, na unaoiona siasa kuwa uwanja unaowahusu zaidi walei wakishirikiana na wananchi wenzao wote.

Tatizo hilo lilikua hasa wakati elimu ilikuwa ya wachache tu, hivyo wasionayo walikosa uwezo wa kutoa hoja zao, na iliwabidi kuendeshwa na wenye elimu, wakiwemo kwa kiasi kikubwa baadhi ya wakleri.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mfumokleri kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.