Mdudu-gamba
Mdudu-gamba | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mdudu-gamba mwororo kijani (Coccus viridis)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Familia 39:
|
Wadudu-gamba au wadudu magamba ni wadudu wadogo wa familia ya juu Coccoidea katika oda Hemiptera ya nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Spishi nyingi ni sumbufu, hususa kama wadudu wakiwa tele juu ya mimea, kwa sababu wanafyonza utomvu, kama vidukari na nzi weupe. Lakini hawasambazi virusi kwa sababu hawaendi kutoka mmea mmoja kuelekea mmea mwingine, kama nzi weupe. Hata shida ya kuvu inayokua kwa mana siyo kubwa kuliko shida za vidukari na nzi weupe. Spishi kadhaa hutumika kwa udhibiti wa kibiolojia ili kuua mimea misumbufu, hususa mimea iliyowasili (au kuwasilishwa) kutoka bara jingine. Wadudu-gamba wenyewe huuawa na wadudu wengine, kama wadudu-kibibi, wadudu mabawa-vena, nyigu wa kidusia n.k. Pia kuna kuvu viuawadudu (entomopathogenic fungi) inayoambukiza wadudu hawa, kama Beauveria bassiana, Lecanicillium lecanii na Aschersonia marginata.
Wadudu-gamba ni wadogo. Kwa kawaida kiwiliwili chao kina urefu wa mm 1-5, lakini spishi za familia kadhaa ni kubwa zaidi, hata mpaka mm 35. Majike huchoza kifuniko cha nta ambacho kinaweza kikubwa kuliko mdudu mwenyewe. Kifuniko hiki kinafanana mara nyingi na gamba la samaki au reptilia (asili ya jina lao), lakini nta inaweza kutoka kama nyuzi nyeupe nyembamba, kama kwa Pseudococcidae (vidukari-sufu). Majike hawana mabawa na wale wa spishi nyingi hawana miguu. Kinyume na hawa madume ya spishi zote wana miguu, na pengine mabawa pia, kwa sababu wanaihitaji ili kutafuta majike. Kwa kweli majike huhifadhi umbo wa lava ambayo huitwa neotenia (neoteny). Kama madume wakiwa na mabawa yale ya nyuma yamepungua, mara nyingi mpaka alama tu.
Wakitoka mayai lava wana miguu. Wanatembea kidogo ili kufika mahali pazuri pa kufyonza. Kwa spishi kadhaa upepo hubeba lava kuelekea mmea mwingine. Mara nyingi sisimizi wanawapeleka lava kwenye mahali pazuri, k.m. chipukizi kipya. Katika spishi nyingi mara ya kwanza ambapo lava anaambua anapoteza miguu, isipokuwa madume.
Spishi zilizochaguliwa
[hariri | hariri chanzo]- Aonidiella aurantii, Mdudu-gamba Mwekundu (Red scale)
- Aulacaspis tubercularis, Mdudu-gamba wa Mwembe (Mango scale)
- Ceroplastes rusci, Mdudu-gamba Nta-pinki (Fig wax scale)
- Coccus hesperidum, Mdudu-gamba Mwororo Kahawia (Soft brown scale)
- Coccus viridis, Mdudu-gamba Mwororo Kijani (Sort green scale)
- Icerya purchasi, Mdudu-gamba Takia-pamba (Cottony cushion scale)
- Lepidosaphes beckii, Mdudu-gamba Mzambarau (Purple scale)
- Saissetia coffeae, Mdudu-gamba wa Mbuni (Hemispherical scale)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Coccidae (Mdudu-gamba mwororo kahawia)
-
Dactylopiidae (Mdudu-gamba wa dungusi)
-
Diaspididae (Mdudu-gamba mzambarau)
-
Eriococcidae (Eriococcus coriaceus pamoja na sisimizi)
-
Halimococcidae (Mdudu-gamba wa mkadi)
-
Kermesidae (Kermes echinatus)
-
Kerriidae (Kerria lacca)
-
Lecanodiaspididae (Lecanodiaspis prosopidis)
-
Margarodidae (Porphyrophora hamelii)
-
Monophlebidae (Mdudu-gamba takia-pamba pamoja na lava wa hatua ya kwanza)
-
Ortheziidae (Orthezia urticae)
-
Pseudococcidae (Kidukari-sufu wa mchungwa: majike na dume)