Mbamba Bay
Mbamba Bay | |
Majiranukta: 11°17′10″S 34°48′5″E / 11.28611°S 34.80139°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Ruvuma |
Wilaya | Nyasa |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 13,463 |
Mbamba Bay ni kata na makao makuu ya Wilaya ya Nyasa katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Maana ya Mbamba Bay ni neno Mbamba ambalo ni jina la mlima uliopo eneo la Zambia na Bay, kama inavyojulikana, ni eneo la bahari lililoingia ndani kama Oyster Bay, Mnazi Bay n.k.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 13,463 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012, kata ya Mbamba Bay ilikuwa na wakazi wapatao 10,066 waishio humo. [2]
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Mji wa Mbamba Bay uko kwenye ufuko wa Ziwa Nyasa takriban km 20 upande wa kaskazini wa mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji.
Usafiri
[hariri | hariri chanzo]Kuna bandari inayohudumiwa na meli SV Songea. Kwa ratiba isiyofuatwa mara kwa mara kuna mawasiliano pia na Nkhata Bay huko Malawi, ng'ambo ya ziwa, halafu kwa bandari nyingine za mwambao wa Kitanzania za Ziwa Nyasa hadi Itungi Port.
Kulikuwa na majadiliano ya kujenga reli Mbamba Bay - Mtwara kwa ajili ya usafiri mfupi kati ya Malawi na Bahari Hindi na pia kwa kuboresha maendeleo kusini mwa Tanzania (Mtwara Development Corridor).
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Nyasa - Mkoa wa Ruvuma - Tanzania | ||
---|---|---|
Chiwanda | Kihagara | Kilosa | Kingerikiti | Linga | Liparamba | Lipingo | Lituhi | Liuli | Liwundi | Luhangarasi | Lumeme | Mbaha | Mbambabay | Mipotopoto | Mpepo | Mtipwili | Ngumbo | Tingi | Upolo |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mbamba Bay kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |