Majadiliano:Siku
Nauliza juu ya matumizi ya neno "sekondi" na "sekunde." Lipi hasa tunatumia na kwanini?-- Ndesanjo 25 Agosti 2007
Asante kwa swali. Nisipokosei umbo la kikamusi ni "sekunde". Neno limeingia kupitia Kiingereza. Hapo Kiswahili hakina utaratibu kamili jinsi ya kuingiza maneno haya. Mfano: "sekunde" (second - kama Kijerumani "Sekunde") - lakini shule ya "sekondari" (secondary). Nilipoandika "Sekondi" nilifuata kawaida ya kuingiza maneno ya Kiingereza katika Kiswahili, lakini si lugha sanifu katika mfano huu ninavyotambua baada ya ya kuchungulia swali lako. Basi nimekaa miaka saba Kenya, na Wakenya wengi wasingeuliza swali lako.
Katika makala mengi njia yangu imekuwa kuandika makala kwa umbo la Kiswahili sanifu (hata kama nimekosea bila shaka hapa na pale) na kuweka "redirect" kutoka tahijia tofauti za neno hili. Hivyo utaona ya kwamba nimehamisha makala kwa "sekunde" na kuweka viungo vya "redirect" kutoka sekondi, sekundi na nukta. Hivi vitasaidia kama umbo tofauti latumiwa katika makala mengine.
Naomba tuendelee kushauriana. --Kipala 22:51, 25 Agosti 2007 (UTC)