Lecrae
Lecrae | |
---|---|
Lecrae na Akon, mnamo 2013
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Lecrae Moore |
Aina ya muziki | Kikristo, Nyimbo za Kikristo |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Studio | Reach Records |
Tovuti | http://www.reachrecords.com/ |
Lecrae Moore (amezaliwa 9 Oktoba, 1979) ni msanii wa Kikristo[1] mwenye mkataba na Reach Records.[2]
Lecrae anaishi mjini Atlanta, Georgia akiandaa matukio mbalimbali ya muziki, akijitolea kufanya kazi katika jela ya vijana, kujishirikisha katika shirika la Kids Across America Kamps huko Branson, Missouri na akijishughulisha na Reachlife Ministries.[3] Pia, yeye ni mwanachama wa 116 Clique, Lecrae anahubiri Injili katika vyuo vikuu mbalimbali na kumbi mbalimbali za jamii.
Lecrae amepokea uchaguzi wa kuwa mshindani kwa tuzo mbili katika tuzo za kila mwaka za GMA Dove. Alipata uchaguzi kwa wimbo wake Jesus Muzik,aliomshirikisha Trip Lee na kwa albamu yake After the Music Stops[4]. Yeye ,hivi majuzi,alikuwa amechaguliwa kama mshindani kwa tuzo ya Albamu ya Sanaa ya Rap ya Mwaka katika tuzo za arubaini za GMA Dove. Magazeti mbalimbali,likiwemo Rapzilla[5] yameaona na kusifu mtindo wake tofauti na albamu yake ya pili After the Music Stops iliitwa "mojwapo ya albamu bora sana ya 2006[6]". Nyimbo zake zinaonyesha werevu wake lakini zinahakikisha ujumbe umewasilishwa.
Katika muziki wake, Lecrae anatumia neno "Crunk" kwa kumaanisha hisia nzuri anayohisi Mkristo.[7] 8 Oktoba 2008, albamu ya tatu ya Lecrae, Rebel, iliingia chati ya Billboard ikwa # 60,huku ikiwa imenunuliwa na watu 9,800. Rebel ikawa # 3 katika iTunes na kushikilia nafasi ya kwanza katika chati ya Kikristo ya Billboard kwa wiki mbili,albamu ya rap ya kwanza kufanya hivyo. Lecrae ana video nne vya nyimbo zake:Jesus Muzik, Praying For You, Don't Waste Your Life, ambayo ilishinda Video ya Mwaka katika tuzo za GMC na hapo Oktoba 2009 alitoa video ya wimbo wake Go Hard.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Miaka ya awali (2003 -2005)
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa Houston, Texas na akalelewa na mama pekee bila baba, alikuwa Mkristo akiwa na umri wa miaka 19. Lecrae alianza kuimba juu ya imani yake na kuwa mwanzilishi wa Reach Records akiwa na umri wa miaka 25. Mwaka 2005, alitoa albamu yake ya Real Talk[8] The album gained critical acclaim and charted at #29 on the Billboard Gospel albums chart.[9] kwa kurekodia huko Reach Records.[10] Albamu hiyo ilipata sifa ikawa #29 kwenye chati ya Billboard ya albamu za Kikristo.[11]
After The Music Stops (albamu) (2006-2007)
[hariri | hariri chanzo]Baada ya ufanisi wa Real Talk,Lecrae alitoa albamu yake ya pili ya studio mnamo 15 Agosti ,2006,albamu hiyo ilikuwa #5 katika chati ya Billboard ya albamu za Kikristo na #16 katika chati ya Billboard Heatseeker.[12] Albamu hii ilichaguliwa kuwa mshindani katika tuzo ya Dove na vilevile wimbo wake Jesus Musik ulichaguliwa.
Rebel (albamu) (2008-2009)
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 8 Oktoba 2008, albamu ya tatu,Rebel, iliingia chati ya Billboard katika nafsi ya 60 ikiwa imenunuliwa na watu 9,800.Albamu hiyo ilipata sifa nyingi kabisa kwa muziki ya aina hiyo.Jesusfreakhideout ilisema,"Katika ulimwengu wa muziki,albamu hii ni nzuri sana kuliko muziki ya aina hiyo yenye utasikia katika stesheni za redio.Katika utunzi wa nyimbo, Lecrae ana ujumbe mzuri kwako na mtu yeyote." Albamu hii,hivi sasa(Januari 2010),imekuwa katika chati ya BillBoard ya albamu za Kikristo kwa wiki 66.[13]
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Albamu
[hariri | hariri chanzo]- Real Talk (2005)
- After the Music Stops (2006)
- Rebel (2008)
Nyimbo zisizokuwa kwenye albamu
[hariri | hariri chanzo]- "Hands High" (2008)
- "Catch That Wave"(2008)
- "Dream" (2009)
Video zake
[hariri | hariri chanzo]- Praying For you (2006)
- Jesus Muzik (2006)
- "Don't Waste Your Life" (2008)
- "Go Hard" (2009)
Akiwa na 116 Clique
[hariri | hariri chanzo]- The Compilation Album (2005)
- The Compilation Album: Chopped & Screwed (2006)
- 13 Letters (2007)
- Amped (2007)
Nyimbo alizoshirikishwa
[hariri | hariri chanzo]- "No Silence" ya FLAME
- "Stand" ya Da' T.R.U.T.H. akimshirikisha FLAME
- "No More" ya Tedashii
- "In Ya Hood Cypha" ya Tedashii akiwashirikisha Trip Lee, Thi'sl, Json & Sho Baraka
- "Cash or Christ" ya Trip Lee
- "116 Intro (Remix)" ya Trip Lee akimshirikisha Tedashii
- "Give Him Glory" ya Trip Lee
- "National Anthem (Remix)" ya Mark J akimshirikisha Shabach, 2nd Nature, Promise, R-Swift, J Johnson, Truth, Japhia Life & Triumph
- "Everyday All Day Cypha" ya Everyday Process akiwashirikisha The Ambassador, FLAME, Phanatik & R-Swift
- "Conviction" ya Dillon Chase
- "Jesus is Alive" ya Shai linne
- "Catch Me at the Brook" ya Sho Baraka
- "When the Thrill is Gone" ya J.R.
- "Disciple Me (Remix)" ya Cam
- "Joyful Noise" ya FLAME akimshirikisha John Reilly[14]
- "Breatha" ya R-Swift akimshirikisha Mac the Doulos
- "Who He Is" ya Trip Lee akimshirikisha Cam
- "Who Is He" ya Json
- "Punchlines" ya Dry Bonez Live
- "Checkin' For My God" ya The Ambassador akimshirikisha Trip Lee
- "Send Me" Remix ya Red Letter wa Mars Hill Church
- "26's" ya Tedashii
- "I Got Proof" ya Katalyst
- "Transformers" ya Tedashii akimshirikisha Trip Lee
- "Exposed" ya Benjah akimshirikisha Soyé
- Chase Glory akimshirikisha Lecrae " I Was Made To Praise Him "
- "Show off" ya DJ Official akimshirikisha FLAME
- "On My 116" (Tedashii, Sho Baraka, Trip Lee)
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- Alishinda tuzo ya Video Bora ya Hip Hop katika tuzo za GMC [15]
- Kuchaguliwa kama mshindani wa tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka 2009 katika tuzo za GMA Dove [16]
- Kuchaguliwa kama mshindani wa tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka 2007 katika tuzo za GMA Dove [17]
- Kuchaguliwa kama mshindani wa tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka 2007 [17]
- Won Best Male Artist for 2006 by Rapzilla [18]
- Alishinda tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka 2006 ya Rapzilla [18]
- Alishinda tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka 2006 ya Rapzilla [18]
- Alishinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka 2006 ya Rapzilla [18]
Angalia Pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Reach Records Artist Profile - Lecrae
- ↑ "Christian Post - Christian Rap Artists: Don't Waste Your Life". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-11. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ [www.myspace.com/lecrae]
- ↑ "Gospel Music - The 38th Annual GMA Dove Awards – Nominee List - Entertain Your Belief". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-20. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ "GMA Dove Awards Nominations 2009 Are In!". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-27. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ "Review - Lecrae - After the Music Stops". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-02. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ "Now Thats What I Am Talkin About!!! After the Music Stops by Lecrae". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-27. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ http://www.newreleasetuesday.com/artistdetail.php?artist_id=354
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-06. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ http://www.newreleasetuesday.com/artistdetail.php?artist_id=354
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-06. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-06. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-06. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ The Reilly Band
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-09-17. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ "GMA 40th Dove Award Nominees". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-27. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ 17.0 17.1 "GMA 38th Dove Award Nominees". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-02. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
- ↑ 18.0 18.1 18.2 18.3 "Rapzilla's Best of 2006". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-02. Iliwekwa mnamo 2010-01-12.
External links
[hariri | hariri chanzo]- Reach Records
- Lecrae Rebel Ilihifadhiwa 2 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Cross Movement Records
- Lecrae katika tovuti ya Myspace
- Lecrae Video ya "Jesus Muzik" Ilihifadhiwa 11 Mei 2010 kwenye Wayback Machine.
- Lecrae Video ya "Prayin' For You" Ilihifadhiwa 25 Novemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Lecrae Video ya "Don't Waste Your Life" Ilihifadhiwa 3 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Video interview with Lecrae about his life and beliefs (Part 1, Kipande cha 2, Kipande cha 3)
- Bendi la The Reilly
- Lecrae Ilihifadhiwa 3 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.