Kislovakia
Kislovakia | ||||||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kinamzungumzwa nchini: | Slovakia, Ucheki, Vojvodina (kwa 2,79% ya watu) Marekani, Kanada, Australia, Hungaria, Croatia na Ukraine | |||||||||||||||||||||||||
Wazungumzaji: | Milioini 6 | |||||||||||||||||||||||||
Lugha rasmi: | ||||||||||||||||||||||||||
Nchi: | Slovakia | |||||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kiisimu: | ||||||||||||||||||||||||||
|
Kislovakia ni lugha rasmi inayoongelewa nchini Slovakia, nchi iliyopo Mashariki mwa Ulaya. Ni moja kati ya Lugha za Kislavoni, mkusanyiko wa lugha unajumlisha Kirusi, Kipoland na lugha nyingine kadhaa za Mashariki ya Ulaya.
Lugha hii inafanana kabisa na Kicheki, na Wacheki na Wasovakia wanaweza kuelewana vizuri kabisa wakiwa wanazungumza lugha zao. Kipoland na Kisorbia kina fanana kabisa. Kislovakia kinazungumzwa nchini Slovakia na zaidi ya watu milioni 5.
Matamshi
[hariri | hariri chanzo]Kislovakia kinaandikwa kutumia alfabeti za Kilatini, lakini kuna viji herufi fulani ambavyo viji harama maalum (vinaitwa “diacritics”).
Herufi č, š, ž and dž zina sauti kama ile ya Kiingereza katika chin, shin, vision na juice.
Herufi ď, ľ, ň, and ť huitwa “konsonanti nyepesi”. Hutamkwa kwa kukata ulimi juu kabisa ya mdomo.
C, dz na j nazo pia ni nyepesi. C ipo kama ts katika bats, dz ipo kama ds katika rods, na j ipo kama y katika yes.
Ch ipo kama ch katika Kiscoti loch. V ni zaidi ya Kiingereza w.
Herufi b, d, ď, dz, dž, g, h, z, ž hazisikiki pale wakiwa wanamalizia (kwa mfano: 'd' itasikika kama 't').
Alama zake katika irabu (vokali) huonyesha kwamba irabu hutamkwa kwa urefu zaidi: á, é, í, ó, ý ú. Irabu ndefu haifuati katika silabi inayofuata kwa kutumia irabu fupi.
Ile ô ipo kama Kiingereza wombat, na ä ni sawa na herufi e.
Kistress ndiyo inayotumika kuanzishia silabi ya neno. Hii ni tofauti kabisa na Kirusi, kwa mfano, wapi Kistress kinaweza kikawa.
Kama jinsi ilivyo katika lugha zingine za Kislavoni, Kislovakia ni vigumu kwa wazungumzaji wa Kiingereza kuweza kutamka. Hii hasa kwa sababu maneno kadhaa yameambatanisha konsonanti nyingi kuwa pamoja. Katika sentensi: “Strč prst skrz krk!” hakuna hata irabu moja (ina maana: “Zungusha vidole kwenye shingo yako!”)!
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- makala za OLAC kuhusu Kislovakia
- lugha ya Kislovakia katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/slk
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kislovakia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |