Kinyesi cha binadamu
Kinyesi cha binadamu (au kinyesi tu, kutoka kitenzi "kunya"; kwa Kiingereza: feces, kutoka Kilatini: fæx) ni mabaki ya chakula ambayo hayakuweza kufyonzwa au kumeng'enywa ndani ya utumbo mdogo wa binadamu, lakini yameozeshwa na bakteria kwenye utumbo mkubwa[1][2] Pia huwa bakteria na idadi ndogo ya taka za kimetaboliki kama vile bilirubini iliyobadilishwa na bakteria, na seli za epithelial zilizokufa kutoka kwa bitana ya utumbo.[1]. Hutolewa kwa njia ya mkundu wakati wa kujisaidia haja kubwa.
Kinyesi cha binadamu kinafanana na kinyesi cha wanyama na hutofautiana kwa mwonekano (kwa mfano, ukubwa na rangi), kulingana na hali ya chakula, mfumo wa kumeng'enya na afya ya jumla. Kwa kawaida kinyesi cha binadamu ni nusu yabisi, na mpako wa kamasi. Vipande vidogo na vigumu tena vikavu, wakati mwingine vinaweza kuonekana vimeathiriwa kwenye mwisho wa distal (mwishoni au chini). Hili ni tukio la kawaida wakati mmeng'enyo wa awali wa tumbo haujakamilika, na kinyesi hurejeshwa kutoka kwenye puru kwenda kwa utumbo mkubwa, ambapo maji hufyonzwa zaidi.
Kinyesi cha binadamu na mkojo wa binadamu kwa pamoja hujulikana kama taka za kibinadamu. Namna nzuri ya kuhifadhi kinyesi cha binadamu, na kuzuia kuenea kwa vimelea kutoka kwa kinyesi cha binadamu kupitia njia ya kinywa, ndiyo malengo makuu ya usafi wa mazingira.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 Tortora, Gerard J.; Anagnostakos, Nicholas P. (1987). Principles of anatomy and physiology (tol. la Fifth). New York: Harper & Row, Publishers. uk. 624. ISBN 978-0-06-350729-6.
{{cite book}}
: Unknown parameter|name-list-format=
ignored (|name-list-style=
suggested) (help) - ↑ Diem, K.; Lentner, C. (1970). "Faeces". in: Scientific Tables (tol. la Seventh). Basle, Switzerland: CIBA-GEIGY Ltd. ku. 657–60.
{{cite book}}
: Unknown parameter|name-list-format=
ignored (|name-list-style=
suggested) (help)
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kinyesi cha binadamu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |