Nenda kwa yaliyomo

Kiitalia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kiitaliano)
Dante Alighieri (juu) na Petrarca (chini) walichangia sana kufanya lahaja ya Firenze ienee kuanzia karne za kati
Pietro Bembo alisanifu lugha ya Kiitalia kwa kutegemea lahaja ya Toscana

Kiitalia ("lingua italiana" au "italiano") ni lugha inayozungumzwa na watu milioni 85, hasa katika Rasi ya Italia.

Ni lugha rasmi ya Italia, San Marino, Vatikano, Uswisi na katika sehemu za Slovenia na Kroatia.

Inatumika pia katika Monako, Malta, Albania na visiwa kadhaa vya Ugiriki), halafu bado kama lugha ya elimu katika nchi zilizokuwa makoloni ya Italia kama Eritrea, Libya, Ethiopia na Somalia.

Watu wengi wanaokitumia kama lugha mama wamekisambaza katika nchi zote walikohamia, kama vile Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Marekani, Kanada, Brazil, Uruguay, Argentina, Venezuela, Australia n.k.[1]

Ni ya 4 kati ya lugha za kigeni zinazosomwa zaidi duniani, hasa kwa sababu ya umuhimu wake katika ustaarabu, kuanzia muziki, lakini pia katika biashara, k.mf. ya bidhaa za utamaduni wa Italia.

Kihistoria asili yake ni lugha ya Kilatini, hivyo pamoja na Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania na lugha nyingine ndogo ni moja ya lugha za Kirumi. Kati ya lugha hizo, Kiitalia ndicho kinachofanana zaidi na Kilatini, labda baada ya Kisardinia.

Imegawanyika katika lahaja nyingi, hasa za Kaskazini na za Kusini mwa rasi hiyo. Imesanifiwa kwa msingi wa lahaja ya Firenze (mkoa wa Toscana, Italia ya Kati).

Blau: Amtssprache; Hellblau: Verkehrssprache

Kiitalia na uenezi wake

  1. Berloco 2018
  • Simone, Raffaele (2010). Enciclopedia dell'italiano. Treccani.
  • Berloco, Fabrizio (2018). The Big Book of Italian Verbs: 900 Fully Conjugated Verbs in All Tenses. With IPA Transcription, 2nd Edition. Lengu. ISBN 9788894034813.
  • Palermo, Massimo (2015). Linguistica italiana. Il Mulino. ISBN 9788815258847.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]