Kigali
Majiranukta: 1°56′38″S 30°3′34″E / 1.94389°S 30.08634°E | |
Nchi | Rwanda |
---|---|
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 600 000 |
Kigali ni mji mkuu wa Rwanda na pia mji mkubwa kuliko mingine yote nchini.
Iko karibu sana na mstari wa ikweta kwenye kimo cha 1400 - 1600 m juu ya UB. Hali ya hewa ni ya wastani hakuna baridi kali wala joto kali.
Kigali ina wakazi 600,000.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kigali ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani mwaka 1907 kama kituo cha mwakilishi wa Afrika ya Mashariki Mjerumani Richard Kandt. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivamiwa na Wabelgiji ikawa sehemu ya eneo lao na kukabidhiwa Rwanda na Burundi chini ya utawala wa Ubelgiji.
Baada ya kugawa kwa Rwanda-Burundi kuwa nchi mbili za Rwanda na Burundi, Kigali ikawa mji mkuu wa Rwanda mwaka 1962.
Mauaji ya Watutsi ya mwaka 1994 yalianza Kigali. Mji ulipungukiwa wakazi 100,000 wakati ule.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Misingi ya uchumi ya Kigali ni biashara ya kahawa, mifugo na Bustani.
Mawasiliano
[hariri | hariri chanzo]Kigali ina uwanja wa ndege wa kimataifa uitwao Kigali International Airport. Kuna barabara kwenda Burundi na Uganda. Bildung
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kigali kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |