Nenda kwa yaliyomo

Kaunti ya Machakos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuhusu mji, soma Machakos

Kaunti ya Machakos
Kaunti
Ofisi ya gavana wa Machakos
Bendera
Machakos County in Kenya.svg
Kaunti ya Machakos katika Kenya
Coordinates: 01°14′S 37°23′E / 1.233°S 37.383°E / -1.233; 37.383
Nchi Kenya
Namba16
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Mashariki
Makao MakuuMachakos
Miji mingineKangudo, Matuu, Kithimani, Athi River
GavanaDkt. Alfred Mutua, CBS
Naibu wa GavanaENG. Francis Maliti Wambua
SenetaBoniface Mutinda Kabaka
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Joyce Kamene
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Machakos
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa40
Maeneo bunge/Kaunti ndogo8
Eneokm2 6 042.7 (sq mi 2 333.1)
Idadi ya watu1,421,932
Wiani wa idadi ya watu235
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC 3)
Tovutihttp://www.machakosgovernment.com/

Kaunti ya Machakos ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 1,431,932 katika eneo la km2 6,042.7, msongamano ukiwa hivyo wa watu 235 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Machakos. Inatarajiwa kuwa na mji wa Konza ambao ndio mji wa kwanza wa teknohama katika Afrika Mashariki.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Machakos inapakana na Nairobi, Kiambu, Murang'a (magharibi), Embu (Kaskazini), Kitui (mashariki), Makueni na Kajiado(kusini). Tabianchi ya Kaunti ya Machakos ni nusu kavu. Ina mandhari yenye vilima[2]. Udongo katika maeneo mengi ni udongo wa mfinyanzi ulio mwekundu. Hata hivyo, kuna mito ambayo huchimbwa mchanga haramu. Jambo hili huharibu mandhari kwa kukausha mito.

Mto Tana na Mto Athi hupitia katika kaunti hii. Bwawa la Masinga liko kaskazini katika mpaka wa Machakos na Embu.

Kiwango cha ardhi kilicho misitu ni 7.6%. Vyanzo vya maji katika kaunti ni Vilima vya Iveti, Muumandu, Kalimanzalu and Kiima Kimwe.

Machakos hupata misimu miwili ya mvua, Oktoba hadi Disemba na Machi hadi Mei. Maeneo yaliyo na vilima hupata mvua mingi, kiwango cha mm 1000, kuliko maeneo kavu ambayo hupata mvua ya kiwango cha mm 500. Mwezi wa Julai huwa na baridi zaidi.

Kaunti ya Machakos imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[3]:

Eneo bunge Kata
Masinga Kivaa, Masinga ya Kati, Ekalakala, Muthesya, Ndithini
Yatta Ndalani, Matuu, Kithimani, Ikomba, Katangi
Kangundo Kangundo Kaskazini, Kangundo ya Kati, Kangundo Mashariki, Kangundo Magharibi
Matungulu Tala, Matungulu Kaskazini, Matungulu Mashariki, Matungulu Magharibi, Kyeleni
Kathiani Mitaboni, Kathiani ya Kati, Upper Kaewa/Iveti, Lower Kaewa/Kaani
Mavoko Athi River, Kinanie, Muthwani, Syokimau/Mulolongo
Machakos Town Kalama, Mua, Mutitini, Machakos ya Kati, Mumbuni Kaskazini, Muvuti/Kiima-Kimwe, Kola
Mwala Mbiuni, Makutano/Mwala, Masii, Muthetheni, Wamunyu, Kibauni

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]

[hariri | hariri chanzo]
  • Athi River 322,499
  • Kalama 54,462
  • Kangundo 97,917
  • Kathiani 111,890
  • Machakos 170,606
  • Masinga 148,522
  • Matungulu 161,557
  • Mwala 181,896
  • Yatta 172,583

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. "Machakos Government - Official Website". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-04-09. Iliwekwa mnamo 2018-04-18.
  3. "Machakos County". Iliwekwa mnamo 2018-04-18. {{cite web}}: Text "County Trak Kenya" ignored (help)
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.