Kamusi ya Kiswahili Sanifu
Mandhari
(Elekezwa kutoka KKS)
Kamusi ya Kiswahili Sanifu (kifupi: KKS) ni kamusi ya lugha ya Kiswahili iliyotolewa mara tatu na wataalamu wa TUKI (sasa TATAKI) kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Inaorodhesha vidahizo (maneno) kwenye kurasa 646, pamoja na maelezo, orodha ya vibadala, kurasa za picha, jedwali za vivumishi na viwakilishi na orodha ya majina ya nchi.
Kamusi hii inakusanya maneno ya Kiswahili sanifu na kuyaeleza kwa lugha yenyewe ya Kiswahili, ikiongoza kwa Kiswahili sanifu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam, Tanzania: Oxford University Press. 1981.
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kamusi ya Kiswahili Sanifu kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |