Nenda kwa yaliyomo

Jumuiya ya Madola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Jumuiya ya madola)
Jumuiya ya Madola (Commonwealth of Nations)


Bendera ya Jumuiya ya Madola

Lugha rasmi Kiingereza
Katibu Mkuu Don McKinnon (tangu 1999)
Chanzo chake mw. 1926 kama jumuiya ya "Kibritania", tangu 1949 kama Jumuiya ya Madola ya kisasa
Madola wanachama 53
Makao Makuu Westminster, London
Mtandao thecommonwealth.org

Jumuiya ya Madola (jina la Kiingereza ni Commonwealth of Nations) inaunganisha nchi mbalimbali hasa Uingereza na nchi zilizokuwa koloni zake.

Umoja huu umeanzishwa mw. 1926 kama "Jumuiya ya Kibritania" (British Commonwealth) na kupewa jina lake la sasa tangu 1949. Inafuatana na Dola la Kibritania au Dola la Kiingereza ambayo ilikuwa dola kubwa kabisa katika historia ya dunia lakini maeneo yake yalianza kuachana baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kutokana na kudhoofishwa kwa Uingereza vitani na miendo ya kupigania uhuru katika nchi mbalimbali hasa Uhindi.

Leo zipatao asilimia 30 ya watu wote duniani (watu 1,800,000) huishi katika nchi wanachama za Jumuiya ya Madola. Nchi za jumuiya hii wenye wakazi wengi ni hasa Uhindi, Pakistan, Bangladesh na Nigeria. Kuna pia nchi ndogo sana kama Tuvalu yenye wakazi 11,000 pekee.

Nchi kadhaa zilisimamishwa uanachama au kuondoka kwa hiari zao. Mfano Tanganyika na Zanzibar ziliungana kwa hiyo hazipo tena lakini mpya ya Tanzania imekuwa nchi mwanachama. Vilevile Newfoundland iliondoka katika jumuiya baada ya kujiunga na Kanada kama jimbo.

Pakistan ilisimamishwa uanachama mara kadhaa kwa sababu serikali yake ilipinduliwa na wanajeshi walioanzisha serikali ya kijeshi. Imerudishwa tena.

Zimbabwe ilisimamishwa uanachama baada ya uchaguzi bandia 2002 ikaamua kujiondoa kabisa mwaka 2003.

Jamhuri ya Ueire iliamua mwaka 1949 kuacha viungo vyote na Uingereza ikajitangaza kuwa jamhuri isiyokubali athira ya nje kama hali ya malkia wa Uingereza kuwa mkuuw a dola hivyo ikaondoka katika jumuiya.

Afrika Kusini ilijiondoa 1961 kwa sababu ya upinzani wa jumuiya dhidi ya sheria za apartheid. Baada mwisho wa ubaguzi wa rangi nchi ilirudi katika jumuiya.

Fiji imesimamishwa mara kadhaa baada ya uasi wa kijeshi uliopindua serikali.

Nchi wanachama za Jumuiya ya Madola

[hariri | hariri chanzo]
Ilijiunga Nchi Bara Wakazi
1931 Afrika Kusini Afrika 47,423,000
1981 Antigua na Barbuda Amerika ya Kati 81,000
1931 Australia Oceania 20,555,300
1973 Bahamas Amerika ya Kati 323,000
1972 Bangladesh Asia 148,384,000
1966 Barbados Amerika ya Kati 279,000
1981 Belize Amerika ya Kati 287,730
1966 Botswana Afrika 1,765,000
1984 Brunei Asia 374,000
1978 Dominika Amerika ya Kati 79,000
1970 Fiji Oceania 848,000
1965 Gambia Afrika 1,517,000
1957 Ghana Afrika 22,113,000
1974 Grenada Amerika ya Kati 103,000
1966 Guyana South America 751,000
1947 India Asia 1,100,000,000
1962 Jamaika Amerika ya Kati 2,651,000
1995 Kamerun Afrika 16,322,000
1931 Kanada Amerika ya Kaskazini 32,654,500
1963 Kenya Afrika 34,256,000
1961 Kipro Ulaya 818,200
1979 Kiribati Oceania 99,000
1966 Lesotho Afrika 1,795,000
1964 Malawi Afrika 12,884,000
1957 Malaysia Asia 27,356,000
1982 Maldivi Asia 329,000
1964 Malta Ulaya 402,668
1968 Morisi Afrika 1,245,000
1995 Msumbiji Afrika 19,792,000
1990 Namibia Afrika 2,031,000
1968 Nauru Oceania 14,000
1931 New Zealand Oceania 4,147,972
1960 Nigeria Afrika 132,796,000
1947 Pakistan Asia 158,352,000
1975 Papua Guinea Mpya Oceania 5,887,000
1983 Saint Kitts na Nevis Amerika ya Kati 43,000
1979 Saint Lucia Amerika ya Kati 161,000
1979 Saint Vincent na Grenadini Amerika ya Kati 119,000
1970 Samoa Oceania 185,000
1976 Shelisheli Afrika 81,000
1961 Sierra Leone Afrika 5,525,000
1965 Singapur Asia 4,326,000
1978 Solomon Islands Oceania 478,000
1948 Sri Lanka Asia 20,743,000
1964 Tanzania Afrika 50,329,000
1970 Tonga Oceania 102,000
1962 Trinidad na Tobago Amerika ya Kati 1,305,000
1978 Tuvalu Oceania 10,000
1962 Uganda Afrika 28,816,000
1931 Ufalme wa Maungano (Uingereza) Ulaya 60,209,500
1968 Uswazi Afrika 1,032,000
1980 Vanuatu Oceania 211,000
1964 Zambia Afrika 11,668,000

Nchi wanachama za zamani

[hariri | hariri chanzo]
Ilijiunga Nchi Bara Ilitoka
1931 Ueire Ulaya 1949
1931 Newfoundland Amerika ya Kaskazini 1949
1961 Tanganyika Afrika 1964
1963 Zanzibar Afrika 1964
1980 Zimbabwe Afrika 2003

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]