Israeli (maana)
Mandhari
Israeli ni jina linalotaja
- Nchi ya Israeli ya kisasa
- Israeli ya Kale ambayo ni nchi au pia jumuiya ya watu ambao historia yao husimuliwa katika Biblia.
- Watu wa Biblia wanaotajwa katika Tanakh au Biblia ya Kiebrania; kwa hiyo pia katika Agano la Kale tena katika Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo
- Yakubu mwana wa Isaka mwana wa Ibrahimu (Abrahamu) alipewa jina la Israeli baada ya kushindana na Mungu (tazama Mwanzo (Biblia) 32,29 "maana umeshindana na Mungu na watu nawe umeshinda")
- jina la pamoja kwa ajili ya makabila 12 waliotokana na wana 12 wa Yakobo-Israeli, mara nyingine kwa umbo la Wanaisraeli
- jina la milki ya kaskazini ya Israeli (milki) iliyoanzishwa baada ya kifo cha mfalme Suleimani kando ya milki ya Yuda; historia ya hizo mbili kwa jumla hujadiliwa chini ya jina "Israeli ya Kale".
- Baada ya maangamizi ya milki ya kaskazini katika vita dhidi ya Waashuri jina lilitumiwa kwa ajili ya watu wa milki ya kusini yaani watu wa milki ya Yuda
- Baada ya maangamizi ya milki hiyo pia jina lilitaja Wayahudi kama jumuiya ya kidini na taifa lililokaa katika sehemu mbalimbali (linganisha matumizi katika Agano Jipya kwenye Waraka kwa Waroma 9,6 na 11,25)
- Kwa kutaja Wayahudi jina latumiwa katika Qurani mara nyingi kama "wana wa Israeli"
- Kwa watu wanaoitwa taifa teule katika Agano la Kale tazama kwa jumla Israeli ya Kale
- Israeli ni pia jina la kawaida la mwanamume kati ya Wayahudi hadi leo