Historia ya Sierra Leone
Historia ya Sierra Leone inahusu eneo la Afrika Magharibi ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Sierra Leone.
Nchi yenyewe ilianzishwa na Waingereza kwa kuunda mji wa Freetown ("Mji wa watu huru") mwaka 1787. Kusudi ilikuwa kuwarudisha Afrika watu waliowahi kuwa watumwa. Kiasili wale wakazi wa kwanza walikuwa watumwa weusi waliopewa uhuru kwa sababu walishikamana na Waingereza dhidi ya Wamarekani katika vita vya uhuru wa Marekani.
Baadaye Waingereza wapinzani wa utumwa walinunua watumwa wakiwapa uhuru na kuwapeleka Sierra Leone.
Tangu mwaka 1807 Uingereza ulikataza biashara ya watumwa (lakini utumwa wenyewe bado) na watumwa waliopatikana kwenye meli za biashara hiyo haramu walipelekwa Sierra Leone na kupewa uhuru.
Ikianzishwa na shirika la wapinzani wa utumwa Sierra Leone ikawa koloni la kwanza la Uingereza katika Afrika ya Magharibi mwaka 1792. Kuanzia mwaka 1802 Freetown ilikuwa makao makuu ya Kiingereza kwa Afrika ya Magharibi.
Mwaka 1961 Sierra Leone ilipewa uhuru wake.
Miaka 1994 - 2002 nchi ilikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tangu mwisho wake nchi inajengwa tena.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Sierra Leone kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |