Historia ya Libya
Historia ya Libya inahusu eneo la Afrika Kaskazini ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Libya.
Wakazi asili walikuwa Waberber. Baadaye wakaja Wafoinike upande wa magharibi na Wagiriki upande wa mashariki.
Hatimaye Libya ikamezwa na Dola la Roma, na Ukristo ukaenea.
Baada ya dola hilo kuanguka, Wavandali waliteka sehemu kubwa ya nchi.
Katika karne ya 7 Waarabu waliingiza Uislamu na utamaduni wao.
Mwaka 1551 Waturuki walifukuza Wazungu kutoka Tripoli wakatawala hadi karne ya 20.
Nchi ilitawaliwa na Waitalia tangu mwaka 1911 hadi 1941 ilipotekwa na Waingereza ambao, baada ya Vita vikuu vya pili kwisha, waliacha nchi mwaka 1951 mikononi mwa mfalme mwenyeji Idris I, aliyekuwa amepinga ukoloni tangu mwaka 1920 (Vita vya Libya dhidi ya Italia).
Kisha kumpindua mfalme huyo, Muammar al-Gaddafi alitawala kidikteta tangu mwaka 1969 hadi alipopinduliwa na kuuawa mwaka 2011 kwa mkono wa N.A.T.O..
Baada ya hapo wananchi wanazidi kupigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mwaka 2020 kulikuwa na makubaliano ya kusimamisha vita na kuunda serikali ya pamoja ili kuandaa uchaguzi mkuu ambao lakini unachelewa kufanyika.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Libya kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |