Himid Mao
Maelezo binafsi | |||
---|---|---|---|
Jina kamili | Himid Mao Mkami | ||
tarehe ya kuzaliwa | 5 Novemba 1992 | ||
mahali pa kuzaliwa | Dar es Salaam, Tanzania | ||
Maelezo ya klabu | |||
Klabu ya sasa | Ghazi El-Mahalla | ||
Senior career* | |||
Miaka | Timu | Apps† | (Gls)† |
2008–2018 | Azam | ||
2018–2019 | Petrojet | 30 | (1) |
2019-2021 | ENPPI | 44 | (1) |
2021- | Ghazl El Mahalla | 51 | (2) |
Timu ya Taifa ya Kandanda‡ | |||
– | Tanzania chini ya miaka 17 | ||
– | Tanzania | 61 | (2) |
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only. † Appearances (Goals). |
Himid Mao Mkami (alizaliwa Dar es Salaam, Tanzania, 5 Novemba 1992) ni mchezaji wa kimataifa kutokea nchini Tanzania anayecheza nafasi ya kiungo katika klabu ya Ghazl El Mahalla inayoshiriki ligi kuu ya nchini Misri na Timu ya Taifa ya Tanzania.[1]
Maisha ya Awali
[hariri | hariri chanzo]Baba yake, Mao Mkami, alikua pia mchezaji wa mpira wa miguu na aliiwakilisha Timu ya Taifa ya Tanzania kati ya 1991 na 1995, alifahamika zaidi kwa jina la "Ball Dancer". Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Kiwandani, Turiani, Morogoro, baadae alihamia Karume Dar es Salaam ambapo alisoma mpaka darasa la Sita. Alimaliza elimu yake ya msingi shule ya Msingi Omal Ali Juma iliyopo Magomeni, Dar es Salaam na baadae akajiunga na Shule ya Sekondari Tabata ambapo alihitimu kidato cha nne mwaka 2011.[2]
Kazi ngazi ya Klabu
[hariri | hariri chanzo]Mao alianza kucheza ngazi ya shule za michezo mwaka 2005, na baadaye kuhamia Azam Academy mwaka 2007, hii ni baada ya kuonekana katika timu ya taifa ya umri chini ya miaka 17, akiwa Academy ya Azam, alishinda taji la Uhai Cup mara mbili mfululizo. Mwaka 2008, alicheza mchezo wake wa kwanza wa dhidi ya Kagera Sugar, na baadaye alipandishwa kwenda timu ya Azam, hii ilikua mwaka 2009. Msimu wa 2013–14, alifunga goli dhidi ya Ruvu Shooting na kuisaidia Azam kubeba taji la ligi kwa mara ya kwanza kwenye historia ya mashindano hayo.[3]
Alijiunga na klabu ya Petrojet SC inayocheza ligi kuu nchini Misri baada ya kuitumika Azam kwa misimu 11, hii ilikua ni Juni 2018.[4]Katika msimu wake wa kwanza kwenye klabu hiyo, alicheza michezo 30 kati ya 34.[5] Klabu ya Petrojet iliposhuka daraja, Mao alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya ENPPI SC tarehe 1 Agosti 2019.[6]
Kazi Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Mao alitajwa kwa mara ya kwanza kwenye kikoisi cha timu ya taifa kwa vijana chini ya miaka 17 mwaka 2010 kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Copa Coca Cola nchini Afrika Kusini. Tanzania ilifunga magoli 32 ngazi ya makundi, iliruhusu kufungwa magoli matatu tu, matoke ohayo yalipelekea Tanzania kufuzu hatua ya mitoano. Walitolewa hatua ya robo fainali kwa kupoteza 1 – 0 dhidi ya Botswana.[7] Mao alizichezea pia timu za taifa za umri chini ya miaka 20 na 23.[2]
Mnamo 15 Julai 2017, alifunga goli lake la kwanza ngazi ya kimataifa kwenye mchezo dhidi ya Rwanda ambao uliisha kwa suluhu ya 1–1, mchezo huu ulikua wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON yam waka 2018 kwa nchi za ukanda wa CECAFA.[8]
Mnamo 13 Juni 2019, Mao alitajwa kwenye orodha ya wacheza watakaoshiriki michuano ya AFCON ya mwaka 2019 nchini Misri.[9]
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Klabu
[hariri | hariri chanzo]- As of 29 Aprili 2023[10]
Klabu | Msimu | Ligi | Kombe | Nje ya Bara | Mengineo | Jumla | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Division | Idadi ya Michezo | Magoli | Idadi ya Michezo | Magoli | Idadi ya Michezo | Magoli | Idadi ya Michezo | Magoli | Idadi ya Michezo | Magoli | ||
Petrojet | 2018–19 | Egyptian Premier League | 30 | 1 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 30 | 1 |
ENPPI | 2019–20 | Egyptian Premier League | 22 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 22 | 0 |
2020–21 | Egyptian Premier League | 22 | 1 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 22 | 1 | |
Jumla | 44 | 1 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 44 | 1 | ||
Ghazl El-Mahalla | 2021–22 | Egyptian Premier League | 31 | 2 | 2 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 33 | 2 |
2022–23 | Egyptian Premier League | 20 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 20 | 0 | |
Jumla | 51 | 2 | 2 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 53 | 2 | ||
Career Jumla | 125 | 4 | 2 | 0 | 0 | 0 | 0 | 0 | 127 | 4 |
- Notes
Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]- As of matches played 24 March 2023[11]
Timu ya Taifa | Year | Idadi ya Michezo | Magoli |
---|---|---|---|
Tanzania | 2013 | 5 | 0 |
2014 | 5 | 0 | |
2015 | 10 | 0 | |
2016 | 5 | 0 | |
2017 | 17 | 2 | |
2018 | 6 | 0 | |
2019 | 2 | 0 | |
2020 | 1 | 0 | |
2021 | 2 | 0 | |
2022 | 4 | 0 | |
Jumla | 57 | 2 |
Magoli timu ya Taifa
[hariri | hariri chanzo]- Scores and results list Tanzania's goal tally first.[11]
No | Tarehe | Uwanja | Mpinzani | Magoli | Matokeo | Mashindano |
---|---|---|---|---|---|---|
1. | 15 Julai 2017 | Uwanja wa Michezo wa CCM Kirumba, Mwanza, Tanzania | Rwanda | 1–1 | 1–1 | Kufuzu Chan mwaka 2018 |
2. | 7 Disemba 2017 | Kenyatta Stadium, Machakos, Kenya | Kigezo:Country data ZAN | 1–0 | 1–2 | Kombe la CECAFA 2017 |
Mataji
[hariri | hariri chanzo]Klabu
[hariri | hariri chanzo]- Azam
- Ligi Kuu Tanzania Bara (1): 2013–14
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Himid Mao Mkami". www.365scores.com. Iliwekwa mnamo 2023-04-27.
- ↑ 2.0 2.1 "Ball Dancer JR…Himid Mao Mkami", 28 November 2012. Retrieved on 24 June 2019. (sw)
- ↑ Mavala, Peter (11 Novemba 2017). "Huyu ndiye Himid Mao Mkami". mavalapeter1.blogspot.com. Iliwekwa mnamo 24 Juni 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Tanzania international Himid Mao completes move to Petrojet", 1 June 2018. Retrieved on 24 June 2019.
- ↑ "Petrojet suffer first-ever relegation following Arab Contractors draw", 4 June 2019. Retrieved on 24 June 2019.
- ↑ "Himid Mao joins Shiza Kichuya's former club", 1 August 2019. Retrieved on 2 August 2019. Archived from the original on 2019-08-02.
- ↑ "Botswana shocks Tanzania to reach COPA semis", Mmegi, 9 June 2010. Retrieved on 24 June 2019.
- ↑ "Tunawakati Mgumu mchezo wa Marudiano dhidi ya Rwanda.", 16 July 2017. Retrieved on 24 June 2019. (sw) Archived from the original on 2019-06-24.
- ↑ "Egyptian Premier League duo called-up by Tanzania for AFCON", 13 June 2019. Retrieved on 24 June 2019.
- ↑ Kigezo:Soccerway
- ↑ 11.0 11.1 Himid Mao at National-Football-Teams.com
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Himid Mao kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |