Nenda kwa yaliyomo

Ngole

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Gangawia)
Ngole
Kichwa cha ngole
Kichwa cha ngole
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Colubridae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Colubrinae
Jenasi: Dispholidus
Fitzsimons & Brain, 1958
Spishi: D. typus
(Smith, 1829)
Ngazi za chini

Nususpishi 3:

Ngole, gangawia, sukutu, nyoka-kima (Unguja) au peku (Unguja) (jina la kisayansi: Dispholidus typus) ni spishi ya nyoka-miti wenye rangi ya majani au kahawia katika familia Colubridae. Anatokea katika Afrika kusini kwa Sahara.

Nyoka huyu ni mrefu kiasi, kwa wastani sentimeta 100-160 lakini anaweza kufika zaidi ya sm 180. Kichwa chake kina umbo wa yai na macho makubwa. Magamba ya mgongo ni membamba na yana miinuko mikubwa kiasi. Rangi ya madume ni kijani na kingo za magamba ni nyeusi au buluu, lakini majike wanaweza kuwa kahawia. Kuna namna nyeusi pia.

Chonge ni majozi matatu ya meno nyuma katika taya la juu, chini ya macho. Ngole ni hatari kabisa baina ya nyoka wa Colubridae, kwa sababu wana mg 1.6-8 za sumu na wanaweza kufungua mdomo kwa nyuzi 170 waking'ata. Kwa hivyo wanaweza kuingiza sumu ya kutosha kuua mtu mzima. Hata hivyo sumu hii inafanya kazi yake polepole na dalili zinaonekana baada ya masaa mengi. Ndiyo sababu mhanga ana muda wa kutosha wa kufika hospitali na kupata makata. Hata hivyo watu wanaweza kufikiri kwanza kwamba hawakupata sumu na dalili zikionekana wamechelewa kutafuta makata. Sumu ni toksinidamu ambayo inazuia damu isigande na kusababisha uvujaji damu wa ndani na wa nje. Kwa bahati nzuri nyoka huyu hashambulii kwa kawaida na anahiari kujificha au kutimuka. Akitishwa anaweza kujiinua na kupanua shingo kama fira.

Ngole huishi mitini na hukiakia mchana. Hula vinyonga na mijusi wengine na vyura hasa lakini mamalia wadogo, ndege na mayai pia.

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ngole kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.