GEOnet Names Server
Mandhari
GEOnet Names Server ni seva katika intaneti inayounganisha mkusanyiko wa data kutoka taasisi ya National Geospatial-Intelligence Agency ya jeshi la Marekani na taasisi nyingine ya serikali ya Marekani inayoitwa United States Board on Geographic Names. Data hizi huwa na majina ya mahali milioni sita kote duniani[1].
Data zinapatikana kwa mtu yeyote zinasaidia kutafuta mahali kwenye ramani ya Dunia kwa umakini wa wastani; data za kijeshi zimefupishwa kwa dakika za tao.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Cartographic Users Advisory Council (CUAC) (26–27 April 2007). 2007 Agency Presentation Minutes. Reston, VA: US Geological Survey