Nenda kwa yaliyomo

Esther Kamatari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Esther Kamatari
Alizaliwa 30 Novemba 1951
Nchi Burundi
Kazi yake Mwandishi
Ndoa Ameolewa
Watoto Wawili

Princess Esther Kamatari (alizaliwa 30 Novemba 1951 mjini Bujumbura).[1] ni mwandishi, mwanamitindo na binti wa kifalme wa Burundi aliyehamishwa.[2]

Esther Kamatari alikulia nchini Burundi kama mwanafamilia wa familia ya kifalme. Alisoma katika l'Ecole Nationale d'Administration du Burundi.Kutokana na nchi kupata Uhuru Utawala wa kifalme ulipinduliwa mwaka 1962 katika mapinduzi ya kijeshi na utawala wa kifalme ukafutwa mwaka wa 1966. Kamatari aliikimbia nchi mwaka wa 1970 baada ya kuuawa kwa Baba yake na kwenda kuishi Paris ambako alikua mwanamitindo wa kwanza wa Kiafrika nchini Ufaransa.[3] Jaribio la kusimamisha tena utawala wa kifalme nchini humo lilishindikana baada ya mauaji ya Mfalme Ntare V mnamo 1972.

Historia ya Burundi baada ya uhuru imetawaliwa na mivutano mingi kati ya Wahutu walio wengi na Watutsi walio wachache.Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya 1990 nchini Burundi na migogoro na nchi jirani na masaibu ya maelfu ya watoto wahanga wa vita vilimfanya ajihusishe na Chama cha Watu wa Burundi nchini Ufaransa.Nchini Burundi anajulikana kwa kazi yake ya kujihusisha na masuala ya kijamii.[4]

Kutokana na usimamizi wa Amani wa Afrika Kusini imewezesha uchaguzi nchini Burundi na Esther Kamatari na chama chake cha Abahuza ambayo ina maana ya "kuwaleta watu pamoja," watashiriki kwenye jukwaa la kurejesha utawala wa kifalme.[5]

Esther ameolewa na Mfaransa anayeitwa Gilles ambaye ni daktari. Wana watoto wawili Jade na Arthur. Lakini Esther tayari alikuwa na binti anayeitwa Frédérique kutoka kwenye mahusiano ya awali.[6]

Ufadhili

[hariri | hariri chanzo]
  • Rais wa Chama cha Watu wa Burundi nchini Ufaransa (tangu mwaka 1990).[7]

Machapisho

[hariri | hariri chanzo]
  • Kamatari, E. na Renault, M. 2001. (Hadithi Yangu, Malkia wa Rugo (Princesse des Rugo, mon histoire). Bayard ISBN 2-227-13914-5
  1. https://web.archive.org/web/20180728224716/http://members.iinet.net.au/~royalty/states/africa/burundi.html
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-24. Iliwekwa mnamo 2022-04-02.
  3. https://www.insider.com/how-princess-esther-of-burundi-became-france-first-black-model-2020-6
  4. "Esther Kamatari: The princess who wants to be president". The Independent (kwa Kiingereza). 2004-10-22. Iliwekwa mnamo 2022-04-02.
  5. "afrol News - Burundi princess, top model seeks presidency". www.afrol.com. Iliwekwa mnamo 2022-04-02.
  6. "Burundi Royal Family - THE AFRICAN ROYAL FAMILIES". theafricanroyalfamilies.com (kwa American English). 2022-02-26. Iliwekwa mnamo 2022-04-02.
  7. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-05-04. Iliwekwa mnamo 2022-04-02.