Christina Milian
Christina Milian imeelekezwa hapa. Kwa albamu, tafadhali tembelea Christina Milian (albamu)
Christina Milian | |
---|---|
Christina Milian 2008 akiwa katika sherehe za Billboard na Children Uniting Nations Oscar Party.
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Christine Flores |
Amezaliwa | 26 Septemba 1981 |
Asili yake | Jersey City,, Marekani |
Aina ya muziki | R&B |
Kazi yake | Mwimba Mtunzi Mwigizaji Mnenguaji Mtayarishaji |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 1998–present |
Studio | Def Soul, Island, MySpace |
Tovuti | ChristinaMilian.org |
Christine Flores (amezaliwa 26 Septemba 1981) ni mtunzi, mwimbaji wa muziki wa pop na R&B, mtayarishaji, mnenguaji, na mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Christina Milian. Alizaliwa mjini Jersey City, New Jersey, halafu baadaye akahamia zake mjini Los Angeles. Akiwa na umri wa miaka ipatayo kumi na tatu, Milian akaanza kutamani kuwa mwigizaji.
Milian alipata kutoa albamu yake ya kwanza ya muziki iliyokwenda kwa jina lake mwenyewe, yaani Christina Milian, na wimbo maarufu kutoka katika albamu hiyo ni "AM to PM" na "When You Look at Me".
Nyimbo zote mbili zilipata kushika nafasi ya tatu katika chati bora za muziki wa Ufalme wa Muungano, lakini albamu yake haijapata kuuza nakala nyingi. Albamu ya pili ya Milian ni It's About Time, nayo haijafanikiwa kimauzo, lakini ilipokea Tuzo ya Grammy ikiwa kama albamu bora ya muziki wa R&B.
Wimbo maarufu kutoka katika albamu hiyo ni "Dip It Low", imekuwa nyimbo ya kwanza kwa umaarufu na kutunukiwa na Recording Industry Association of America kuwa kama wimbo bora kwa mauzo ya mtandaoni.
Muziki
[hariri | hariri chanzo]- Christina Milian (2001)
- It's About Time (2004)
- So Amazin' (2006)
- TBA (2009)
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina la filamu | Jina alilotumia | Maelezo mengine |
---|---|---|---|
1996 | Sister, Sister | Lana | Sehemu ya kwanza |
1997 | Smart Guy | "TJ's Friend" | Sehemu mbili |
1998 | A Bug's Life | Sauti ya nyongeza | |
Movie Surfers | Tina Flores | Mfululizo wa kawaida | |
1999 | Durango Kids | Eleanor "Ellie" Bigelow | |
American Pie | Band Geek | Kauza sura | |
The Wood | Msichana aliyekuwa anachezacheza | Kauza sura | |
Clueless | Megan | Sehemu mbili | |
Get Real | Tennisha | Sehemu taru | |
Charmed | Teri Lane | Sehemu moja | |
The Steve Harvey Show | "Young Lady in Hallway" | Sehemu moja | |
The Amanda Show | "Various roles" | Sehemu moja | |
2003 | Wannabes | Host | |
Love Don't Cost a Thing | Paris Morgan | ||
2004 | MTV Cribs | Milian | Sehemu moja |
Torque | Nina | ||
2005 | Man of the House | Anne | |
Be Cool | Linda Moon | ||
2006 | Pulse | Isabell Fuentes | |
2007 | Smallville | Rachel Davenport | Sehemu moja |
Snowglobe | Angela Moreno | TV Movie | |
2008 | Eight Days a Week | Olivia Campbell | Haijarushwa hewani |
Need for Speed: Undercover | Carmen Mendez | ||
2009 | The Ghosts of Girlfriends Past | Bado inatayarishwa | |
Bring it On Cinco | Lina | Bado inatayarishwa |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Official website Archived 2 Januari 2008 at the Wayback Machine.
- Fan website Archived 3 Oktoba 2016 at the Wayback Machine.
- Christina Milian at the Internet Movie Database
- Christina Milian katika YouTube