Nenda kwa yaliyomo

Kaa (mnyama)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Brachyura)
Kaa
Kaa kijiwe
Kaa kijiwe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Crustacea (Arthropoda wenye miguu yenye matawi mawili)
Ngeli: Malacostraca (Crustacea wenye sehemu tatu)
Oda: Decapoda (Crustacea wenye miguu mikumi)
Nusuoda: Pleocyemata
Oda ya chini: Brachyura (Kaa)
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Vitengo 4 na nusu-vitengo 2:

Kaa ni wanyama wa faila Arithropodi, oda Decapoda na oda ya chini Brachyura (brakhys = fupi, oura = mkia) ambao kwa kawaida wana mkia mfupi mno au fumbatio lao limejificha ndani ya kifua. Wanyama wengine wafananao na kaa, kama wanamezi (hermit crabs), kaa-mfalme (king crabs) na kaangao (horseshoe crabs), sio kaa wa kweli. Kaa wamefunikwa na kiunzi cha nje na wana miguu kumi (jozi tano) kama Decapoda wote. Jozi ya kwanza inabeba magando (kucha za kaa).

Kaa wanapatikana katika bahari zote duniani, lakini kaa wengi wanaishi kwenye maji baridi na nchi kavu, hata kwenye sehemu za kitropiki. Kaa wana ukubwa mbalimbali kwa mfano kuanzia pea crab mwenye urefu wa milimita kadhaa, mpaka kwa kaa wa Kijapani (Japanese spider crab wenye mpaka jumla ya urefu (pamoja na miguu yake) wa mita 4. [1]

Mabadiliko na uainishaji

[hariri | hariri chanzo]

Oda ya chini ya Brachyura ina jumla ya spishi 6793 katika familia 93[2], idadi sawa na mabaki ya oda Decapoda[3]. Mabadiliko ya vizazi ya kaa yanajumuisha kuongezeka kwa mwili wenye msuru na kupungua kwa fumbatio. Japokuwa makundi mengine nayo yanapitia mabadiliko hayohayo, kaa wameonekana kuimarika zaidi. Kaa wanafahamika kwa kuhudumia chakula na kulinda familia zao, na wakati wa kujamiiana hutafuta sehemu mzuri ya kaajike kutoa mayai yake.[4]

Kiasi cha spishi 850 [5] za kaa wanaishi kwe maji baridi, au nchi kavu na majini na wanapatikana maeneo mbalimbali hasa maeneo ya kitropiki na nusu tropiki, walionekana kuwa wanauhusiano na wanaunda familia iliyokubwa na karibu sana, lakini sasa inaaminika wanaunda makundi makubwa tofauti mawili, wale wa Dunia Mpya na Dunia ya Kale.

Kaa ni wanyama waliochangamka na wenye tabia tata. Huwasiliana kwa kugonga au kupunga koleo zao. Kaa huchukiana wao kwa wao,na mara nyingi dume huchukiana kuwapata kaa jike. [6] Kwenye fukwe kwenye miamba, ambako mapango na nyufa zimejaa, kaa hupigania pia kupata nafasi.

Kaa hula nyama na majani lakini hasa hula algi [7] na hula chakula kingi chochote kama vile moluski, minyoo, fungi, bacteria, na hata jamii nyingine za crustaceans, kutokana na upatikanaji wao na pia spishi ya kaa husika, kwa kaa wengi, mchanganyiko wa mlo wenye nyama na mimea hupendelea kukua haraka nawenye nguvu htabiti[8][9]

Mapishi ya kaa

[hariri | hariri chanzo]

[[10]] Kaa masala kutoka Karnataka, India

Kaa huandaliwa na kuliwa katika namna mbalimbali sehemu tofauti tofauti za dunia.Baadhi ya spishi wanaliwa wote hata gamba lake, kama vile kaa mwenye gamba laini. Spishi nyingine huliwa miguu yake na koleo lake tu. Hiki ni kitu cha kawaida kwa kaa wa kuliwa kama vile snow crab.

Katika maeneo mbalimbali duniani viungo kadhaa huongezwa kuberesha ladha ya kaa mfano huko Asiai, kaa- masala na kaa- pilipili ni chakula chenye viungo vingi sana.

Kwa Uingereza nyama ya kaa na hupikwa huandaliwa ndani ya magamba ya kaa tena namna mojawapo ya kuandaa kaa wanyama ni kumwondoa na kumwandaa na kumchanganya na unga kutengeneza keki ya kaa.

Kwa kawaida kaa huchemshwa wakiwa hai, wana sayansi wa Norwei walidhihirisha suala hili kwa kusema kuwa kaa hawaumii wala kuhisi maumivu pindi wanapopikwa hivyo. [11], hata hivyo hapo baadae wana sayansi walitambua na kusema kuwa kaa nao huhisi maumivu na kuyakumbuka, japo hili si suala kubwa wakati wa kupika.

[[12]] Wavuvi wakichagua kaa wanaoliwa huko Fionnphort, Scotland

Kaa wanafanya asilimia zaidi ya 20% ya jamii ya crustaceans. Wote wanaovuliwa baharini, na kutumika duniani kote, kufikia tani milioni moja na nusu kwa mwaka.

Kaa na tamaduni

[hariri | hariri chanzo]

[[13]] Moche chombo kikionesha kaa

Kaa ni miongoni mwa alama 12 za kundi la nyoka la zodiaki. John Bevis aliona umbo hilo la kaa na kulifananisha na kaa mnamo 1731.

Picha [[14]] Masked crab

[[15]] Corystes cassivelaunus