Bahari ya Hindi
Bahari ya Hindi ni bahari ya tatu kwa ukubwa duniani ikiwa imechukua asilimia 20 ya uso wa dunia na kuzungukwa na mabara manne.
Upande wa kaskazini imepakana na Asia ya Kusini; magharibi imepakana na Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Shamu na Afrika; mashariki imepakana na Ghuba ya Malay, visiwa vya Sunda (Indonesia), na Australia; na upande wa kusini imepakana na Bahari ya Kusini.
Bahari hii ni njia muhimu ya usafiri na usafirishaji kwa meli kati ya Asia na Afrika.
Jiografia
Mipaka
Mipaka ya Bahari Hindi imeelezwa na Shirika la Kimataifa la Hidrografia kama ifuatayo:
- upande wa magharibi (Atlantiki) ni mstari unaoelekea kusini kutoka Rasi Agulhas (Afrika Kusini) kwenye longitudo ya 20° mashariki
- upande wa mashariki ni mstari unaoelekea kusini kutoka sehemu ya kusini zaidi cha Tasmania (Australia) kwenye longitudo ya 146°55'E
- kati ya Australia na Asia ni mstari wa visiwa vya Indonesia
- upande wa kaskazini ni pwani za Asia na Afrika
- upande wa kusini imeamuliwa kutumia latitudo ya 60°S kama mpaka wa Bahari Hindi na Bahari ya Kusini inayozunguka bara la Antaktiki.
Kwa hiyo eneo lote la uso wa bahari hii ni kilomita za mraba 70,560,000 km²; kina cha wastani ni mita 3,741 ilhali kina kikubwa kinafikia mita 7,906. Mjao wake ni kilomita za ujazo 264,000,000 km³ inayolingana na asilimia 19.8% ya mjao wa bahari zote duniani.
Jiolojia
Chini ya Bahari Hindi kuna mabamba ya gandunia mbalimbali yanayopakana hapa:
Bamba la Antaktiki, Bamba la Afrika, Bamba la Uarabuni, Bamba la Uhindi na Bamba la Australia.
Kama kawaida, pale ambako mabamba yanaachana kuna nafasi inayoruhusu kupanda juu kwa joto na magma kutoka kiini cha dunia na kutokea kwa volkeno pamoja na safu za milima chini ya maji.
Tetemeko la ardhi na tsunami ya 2004, iliyosababisha uharibifu na vifo katika sehemu za kaskazini za Bahari Hindi, ilisababishwa na mwendo wa ghafla la bamba la Australia juu ya bamba la Uhindi.
Bahari za pembeni
Bahari za pembeni, ghuba na hori za Bahari Hindi ni pamoja na:
- Bahari ya Uarabuni
- Ghuba ya Uajemi
- Bahari ya Shamu
- Ghuba ya Oman
- Ghuba ya Aden
- Mlangobahari wa Bab-el-Mandeb (kati ya Bahari ya Shamu na Bahari ya Uarabuni)
- Hori ya Katch
- Hori ya Khambat
- Mlangobahari wa Palk (kati ya Hori ya Bengali na Bahari ya Uarabuni)
- Hori ya Bengali
- Bahari ya Andamani
- Mlangobahari wa Malakka
- Mfereji wa Msumbiji
- Hori Kuu ya Australia
- Bahari ya Timor
- Ghuba ya Mannar
- Bahari ya Lakadivi
Tabianchi
Kwa jumla Bahari Hindi ina halijoto ya juu kulingana na bahari kubwa nyingine za dunia. Tofauti na Atlantiki na Pasifiki haina maeneo makubwa kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia hivyo haipokei baridi kutoka Aktiki.
Upande wa kazkazini wa ikweta kuna monsuni; upepo kutoka kazkazini-mashariki uko kuanzia Oktoba hadi Aprili, kinyume chake upepo kutoka kusini[1] unaendelea kuanzia Mei hadi Oktoba. Badiliko hili linafuata utaratibu wa kila mwaka na lilikuwa msingi kwa usafiri na biashara katika bahari hii maana iliwezekana kutumia upepo kwa jahazi tangu kale.
Wakati wa badiliko la monsuni dhoruba kali zinaweza kutokeas hasa katika Bahari ya Uarabuni na Hori ya Bengali.
Nchi zinazopakana na Bahari Hindi
Asia
Israel na Jordani (kupitia Ghuba ya Akaba na Bahari ya Shamu), Ufalme wa Uarabuni wa Saudia, Yemen, Omani, Falme za Kiarabu, Qatar, Kuwait, Iraq, Iran, Pakistan, India, Bangladesh, Myanmar, Uthai, Malaysia, Indonesia na Timor ya Mashariki.
Australia
Afrika
Afrika Kusini, Msumbiji, Tanzania, Kenya, Somalia, Jibuti, Eritrea, Sudani na Misri (kupitia Bahari ya Shamu).
Nchi za visiwani
Ndani ya Bahari Hindi kuna mataifa huru ambayo ni nchi za visiwani pamoja na Bahrain (Ghuba ya Uajemi), Komori, Madagaska, Maldivi, Morisi, Shelisheli na Sri Lanka.
Indonesia na Timor ya Mashariki ni nchi za visiwani zinazopakana na Bahari Hindi.
Visiwa katika Bahari Hindi
Agalega, Anjouan, Bahrain, Cargados Carajos, Visiwa vya Cocos (Keeling), Diego Garcia, Kilwa Kisiwani, Kirimba (visiwa), Kisiwa cha Mafia, Komori, Kisiwa cha Krismasi, Lamu (kisiwa), Morisi, Madagaska, Mahore, Mahé, Maskarena, Mayotte, Moheli, Msumbiji (kisiwa), Mwali, Ngazija, Pamanzi, Pate, Pemba (kisiwa), Rodrigues (kisiwa), Réunion, Shelisheli, Sokotra, Unguja, Îles Éparses,
Tanbihi
- ↑ "upepo wa kusi" katika lugha ya Waswahili wa pwani
Kujisomea
- Alpers, E. A. (2013). The Indian Ocean in World History. Oxford University Press. ISBN 978-0-19-533787-7.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help); Unknown parameter|layurl=
ignored (help) - Arnsdorf, Isaac. "West Africa Pirates Seen Threatening Oil and Shipping", 22 July 2013. Retrieved on 23 July 2013.
- Brewster, D. (2014). "Beyond the String of Pearls: Is there really a Security Dilemma in the Indian Ocean?". Journal of the Indian Ocean Region. 10 (2). doi:10.1080/19480881.2014.922350. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite journal}}
: Check date values in:|accessdate=
(help); Invalid|ref=harv
(help) - "Oceans: Indian Ocean". CIA – The World Factbook. 2015. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help) - Cabrero, Ferran (2004). "Cultures del món: El desafiament de la diversitat" (PDF) (kwa Portuguese). UNESCO. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help)CS1 maint: unrecognized language (link) - Dreyer, E. L. (2007). Zheng He: China and the Oceans in the Early Ming Dynasty, 1405–1433. New York: Pearson Longman. ISBN 9780321084439.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Eakins, B. W.; Sharman, G. F. (2010). "Volumes of the World's Oceans from ETOPO1". Boulder, CO: NOAA National Geophysical Data Center. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help); Invalid|ref=harv
(help) - El-Abbadi, M. "The greatest emporium in the inhabited world". UNESCO. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help) - Fitzpatrick, S.; Callaghan, R. (2009). "Seafaring simulations and the origin of prehistoric settlers to Madagascar" (PDF). Katika Clark, G. R.; O'Connor, S.; Leach, B. F. (whr.). Islands of Inquiry: Colonisation, Seafaring and the Archaeology of Maritime Landscapes. ANU E Press. ku. 47–58. ISBN 9781921313905. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite book}}
: Check date values in:|accessdate=
(help); Invalid|ref=harv
(help) - Han, W.; McCreary Jr, J. P. (2001). "Modelling salinity distributions in the Indian Ocean" (PDF). Journal of Geophysical Research. 106 (C1): 859–877. doi:10.1029/2000jc000316. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite journal}}
: Check date values in:|accessdate=
(help); Invalid|ref=harv
(help) - "Limits of Oceans and Seas" (PDF). International Hydrographic Organization, Special Publication N°23. 1953. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help) - "The Indian Ocean and its sub-divisions". International Hydrographic Organization, Special Publication N°23. 2002. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help) - Müller, R. D.; Royer, J. Y.; Lawver, L. A. (1993). "Revised plate motions relative to the hotspots from combined Atlantic and Indian Ocean hotspot tracks" (PDF). Geology. 21 (3): 275–278. doi:10.1130/0091-7613(1993)021<0275:rpmrtt>2.3.co;2. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite journal}}
: Check date values in:|accessdate=
(help); Invalid|ref=harv
(help) - Parker, Laura (April 2014). "Plane Search Shows World's Oceans Are Full of Trash". National Geographic News. Iliwekwa mnamo July 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help) - Rais, R. B. (1986). The Indian Ocean and the Superpowers. Routledge. ISBN 0-7099-4241-9.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help) - Roxy, M. K. (2016). "A reduction in marine primary productivity driven by rapid warming over the tropical Indian Ocean". Geophysical Research Letters. 43 (2). doi:10.1002/2015GL066979. Iliwekwa mnamo January 2016.
{{cite journal}}
: Check date values in:|accessdate=
(help)CS1 maint: ref duplicates default (link) - Stow, D. A. V. (2006). Oceans: an illustrated reference. Chicago: University of Chicago Press. ISBN 0-226-77664-6.
- "Tuna fisheries and utilization". Food and Agriculture Organization of the United Nations. 2016. Iliwekwa mnamo January 2016.
{{cite web}}
: Check date values in:|accessdate=
(help); Invalid|ref=harv
(help) |
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|