Nenda kwa yaliyomo

Amri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Amri za Mungu zilizoandikwa kwa Kiebrania juu ya sahani ya kioo.

Amri (kutoka Kiarabu) ni agizo au katazo linalotolewa na mamlaka yoyote kwa watu walio chini yake kwa namna moja au nyingine.

Katika Biblia

[hariri | hariri chanzo]

Katika Biblia ni maarufu Amri Kumi za Mwenyezi Mungu ambaye aliziweka ili asiwepo yeyote wa kuzikaidi, bali kuzishika na kuzitunza katika moyo (Kut 20; Kumb 5). Yesu alionyesha kwamba zote zinajumlishwa katika amri kuu ya upendo kwa Mungu na kwa jirani (Mk 12:28-31). Hatimaye alitoa amri mpya kwamba watu wapendane kama yeye alivyowapenda upeo (Yoh 13:34).

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amri kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.