Nenda kwa yaliyomo

Alexander Fransson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alexander Fransson
binadamu
Jinsiamume Hariri
Nchi ya uraiaUswidi Hariri
Nchi anayoitumikiaUswidi Hariri
Jina halisiAlexander Hariri
Jina la familiaFransson Hariri
Tarehe ya kuzaliwa2 Aprili 1994 Hariri
Mahali alipozaliwaNorrköping Hariri
Kaziassociation football player Hariri
Nafasi anayocheza kwenye timuKiungo Hariri
Muda wa kazi2013 Hariri
Mchezompira wa miguu Hariri
Namba ya Mchezaji15 Hariri
Ameshirikifootball at the 2016 Summer Olympics Hariri

Alexander Fransson (alizaliwa 2 Aprili 1994) ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Uswidi ambaye anacheza kama kiungo wa klabu ya IFK Norrköping.

Kazi ya klabu

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 2 Januari 2016, FC Basel ilitangaza kuwa walikuwa wamemsaini Fransson kwa mkataba wa miaka minne (4) na nusu hadi 30 Juni 2020.

Alicheza ligi kwa mara ya kwanza akiwa na klabu ya Basel tarehe 14 Februari 2016 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Klabu ya Grasshopper akiingia kama mbadala katika dakika ya 90.

Alifunga goli lake la kwanza la ligi akiwa na Basel mnamo 21 Februari wakati wa kushinda nyumbani kwa magoli 5-1 dhidi ya klabu ya Vaduz.Chini ya kocha Urs Fischer,Fransson alisaidia klabu yake kushinda michuano ya Uswisi Super League mwishoni mwa msimu wa 2015-16 na mwishoni mwa msimu wa 2016-17 Super League.Pia walishinda Kombe la Uswisi kwa muda wa miaka kumi na mbili, ambayo ina maana kwamba wameshinda mara mbili ukizidisha na sita kwenye historia ya klabu.

Tarehe 26 Desemba 2017 FC Basel ilitangaza kwamba Fransson atapewa mkopo kwenda katika klabu ya Lausanne-Sport ili kupata uzoefu zaidi wa timu yake ya pili.

IFK Norrköping

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 4 Julai 2018, IFK Norrköping ilitangaza kwamba walikuwa wamemsaini Fransson katika mkataba wa miaka mitatu (3) hadi 30 Juni 2021.

Kazi ya kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Fransson aliwakilisha timu yake ya Taifa chini ya umri wa miaka 19 kati ya mwaka 2012 na 2013. Mnamo Novemba 2014, Fransson alicheza mchezo mechi ya kwanza kwenye Timu ya taifa ya Sweden chini ya umri wa miaka 21.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alexander Fransson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.