Aisha
Aisha bint Abu Bakr (Kar.: عائشة ʿāʾ'isha - mwenye uhai) alikuwa mke wa tatu tena mdogo wa mtume Muhammad.
Utoto
[hariri | hariri chanzo]Aisha alizaliwa Maka akiwa binti wa Abu Bakr. Baba huyu alikuwa rafiki wa karibu wa Muhammad na baadaye khalifa wa kwanza wa Uislamu. Alipokuwa mdogo alimfuata baba aliyekimbia Ethiopia mwaka 615 wakati wa kudhulumiwa kwa Waislamu wa kwanza mjini Maka. Baada ya kurudi aliposwa na Muhammad.
Ndoa
[hariri | hariri chanzo]Aisha aliposwa katika umri mdogo wa miaka 6 au 7. Alipofikia miaka 9 aliolewa kabisa na kuhamia nyumba ya Muhammad huko Madina. Kati ya wake wa mtume anasemekana alikuwa mke wa karibu zaidi naye. Muhammad alipokea ayat nyingi za Qurani wakati alipokuwa na Aisha.
Wasunni waamini ya kwamba Muhammad alipokufa alimtafuta Aisha na kuuaga dunia akilaza kichwa chake mapajani pake. Washia hawakubali wakiamini ya kwamba mtume aliweka kichwa mapajani pake Ali ibn Abi Talib.
Baada ya Muhammad
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kifo cha mtume babake Aisha alikuwa khalifa wa kwanza. Aisha mwenyewe alishiriki katika kazi ya kukusanya kumbukumbu za mtume na hadith zaidi ya 2,000 za Muhammad zimetokana naye.
Alikuwa na nafasi katika siasa ya Uislamu wa kwanza jinsi inavyoonekana katika uasi dhidi ya Ali ibn Abi Talib mwaka 656. Ali alichaguliwa kuwa khalifa wa nne akikataliwa na sehemu ya wandani wa Muhammad. Aisha alikusanya jeshi kati ya watu wa Makka akaelekea Basra alipomshambulia Ali na jeshi lake katika mapigano ya ngamia. Aliposhindwa Alim alimrudisha Madina alipoishi hado kifo chake mwaka 678.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- The Prophet's wives / `A'ishah bint Abi Bakr Archived 20 Oktoba 2006 at the Wayback Machine.