Nenda kwa yaliyomo

Guguye

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Guguye
Bocho domo-jeusi (Lophiomus setigerus)
Bocho domo-jeusi (Lophiomus setigerus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Lophiiformes (Samaki kama mabocho)
Familia: Lophiidae (Samaki walio na mnasaba na guguye)
Rafinesque, 1810
Ngazi za chini

Jenasi 4 na spishi 29, 8 katika Afrika:

Guguye, mabocho au mashinda-dovu ni spishi za samaki washawishi wa baharini wa familia Lophiidae katika oda Lophiiformes wanaopatikana katika Bahari ya Aktiki, ya Atlantiki, ya Hindi na ya Pasifiki. Samaki hawa wanaishi kwenye mchanga au matope ya matako ya bara na miteremko ya matako hayo kwa kina cha m 40 hadi karibu na m 2,000.

Kama wengi wa samaki washawishi wengine wana kichwa kipana sana na kinywa kikubwa kinachobeba meno marefu na makali yaliyopindika nyuma. Pia kama vile samaki washawishi wengine mwiba wa kwanza wa pezimgongo umebadilishwa katika kifaa cha uvuvi kwa mshipi (ilisio, Kiing. illicium) kinachobeba chambo cha umbo wa kibonge chenye nyama (eska, Kiing. esca). Kifaa cha uvuvi kiko kwenye ncha ya pua juu ya kinywa na hutumika ili kuvutia mawindo. Mabocho pia wana miiba miwili au mitatu ya pezimgongo iliyopo nyuma zaidi kichwani na pezimgongo tofauti lenye miiba mmoja hadi mitatu lililopo nyuma zaidi kwenye mwili mbele ya pezi-shahabu. Katika jenasi za asili za mabocho (Sladenia na Lophiodes), miingilio ya matamvua huendelea hadi mbele ya misingi iliyorefuka ya mapeziubavu. Katika jenasi zilizogeuka (Lophiomus na Lophius), na katika samaki washawishi wengine wote, miingilio ya matamvua haiendelei hadi mbele ya misingi ya mapeziubavu. Mabocho wakubwa kabisa huweza kuzidi urefu wa m 1.5.

Spishi kubwa kadhaa za jenasi Lophius, ambazo hujulikana kama "monkfishes" kaskazini mwa Ulaya, ni spishi muhimu zinazovuliwa kibiashara. Ini ya “monkfish”, inayojulikana kama "ankimo", inachukuka kuwa chakula kitamu sana nchini Japani.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Guguye kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.