Ntoro
Ntoro ni sehemu ya kiroho-na-jenetikia ya baba ambayo Waakan wanahisi inarithishwa kwa watoto wake.
Hawa Ntoro 12 wanachukuliwa kama miungu (mioyo) inayorithishwa ambao wanatawala, kuongoza na kulinda makabila yao 12 kwa njia ya baba. Waaan wanahisi kwamba Ntoro haifi pamoja na baba. Badala yake, inarithishwa kwa watoto wa mwanaume, au kama watoto hawapo hai, kwa wapwa na mpwa wake. Ntoro ya baba inawakilisha kuwepo kwa mtoto mpaka mtoto afikie umri wa kujitambua. Katika hatua hii, Ntoro pamoja na Sunsum na Kra inaeleza jinsi mtu anavyoshirikiana katika ulimwengu.[1] Ntoro hivyo hivyo inaelezwa na Waakan kuwa ni tabia na sifa za kiroho za baba ambazo zinaweza kurithiwa. Hivyo basi, ni ushirikiano wa Ntoro ya baba na damu ya mama (Mogya) ya Abusua ambayo inaaminika kuunda mtoto na kumboresha kuwa binadamu.[2]
Tofauti za Ntoro
[hariri | hariri chanzo]1) Bosompra (Ngumu/Imara)
2) Bosomtwe (Binadamu/Mwenye Huruma)
3) Bosomakɔm (Mpenzi wa Kujitolea)
4) Bosompo/Bosomnketia (Shujaa/Kujiamini/Ujasiri)
5) Bosommuru (Mheshimiwa/Anayeheshimika)
6) Bosomkonsi (Mjuzi/Mwenye Uwezo)
7) Bosomdwerɛbe (Mzushi/Mtikisiko)
8) Bosomayensu (Mkali/Mwovu)
9) Bosomsika (Makini/Mchanganuzi)
10) Bosomkrete (Shujaa/Mtukufu)
11) Bosomafram (Mkarimu/Mwenye Huruma)
12) Bosomafi (Mcha Mungu/Pole)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Gyekye Kwame; An essay on African philosophical thought: the Akan conceptual scheme 1995
- ↑ Asante Molefi; African Intellectual Heritage 1996
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |